Mwaka
2013, vuguvugu la Anaconda lilimsaidia Lady Jaydee si tu kukusanya
mashabiki wengi zaidi, bali pia limempa fedha nyingi mno. Hadi sasa
muimbaji huyo ana zaidi ya likes laki mbili kwenye Facebook na followers
zaidi ya 60,000 kwenye Twitter.
Zaidi
ya tiketi 3,500 zilinunuliwa kwenye show yake ya mwezi June ya Miaka 13
ya Muziki na kuingiza takribani shilingi milioni 100. Haikuishia hapo,
album yake Nothing But The Truth ilifanya vizuri na kumfanya kuwa msanii
pekee wa Bongo Flava anayeendelea kufurahia mauzo ya album zake.
Hits
zake mbili, Joto Hasira na Yahaya kutoka kwenye santurui take hiyo,
zimebadilisha maisha yake na kumfanya kuwa mwanamuziki aliyekuwa na show
nyingi zaidi mwaka jana. Lady Jaydee alitumbuiza kwenye karibu show
zote za Kili Music Tour ambako aliiingiza si chini ya shilingi milioni
25.
Mwaka
jana pia Lady Jaydee amefanya show nyingi kubwa ikiwemo ile ya uzinduzi
wa filamu ya Lulu, Foolish Age, show yake kwenye Miss Tanzania 2013,
Family Day Show ya Arusha iliyofanyika Eid Pili, Anaconda Show
iliyofanyika Triple A na nyingine iliyofanyika Snow View Hotel. Akiwa
Arusha pia, Lady Jaydee aliuza kopi za album yake kama njugu pamoja na
t-shirt za Anaconda zilizouzwa kwa shilingi 15,000 kila moja.
June
mwaka jana, Lady Jaydee alitumbuiza kwenye semina ya kuwezesha wanawake
kuondokana na njaa na umaskini, iliyofanyika chini ya mfuko wa fursa
sawa kwa wote chini ya mama Anna Mkapa. Biashara yake ya Nyumbani
Lounge, imeendelea kufanya vizuri pia kwa kupata wateja wengi wanaoenda
kupata chakula, vinywaji na burudani kutoka kwa bendi yake ya Machozi.
Bado
anaingiza fedha kupitia udhamini wa Airtel kwenye show yake ya TV ya
Diary of Lady Jaydee. Msanii huyo ambaye jina lake ni Judith Wambura pia
miongoni mwa wasanii 24 wa bara la Afrika waliochukuliwa kwenye mradi
wa Coke Studio Africa wa kampuni ya Cocacola unaoendelea jijini Nairobi
Kenya. Na sasa Lady Jaydee amekuwa msanii wa Tanzania anayemiliki gari
aghali zaidi, Range Rover Evoque.
“Hakupenda kudisclose mambo ya bei wala wapi alikoinunua,” mume na meneja wa Lady Jaydee, Gadner G Habash ameiambia Bongo5.
“Lakini
tunashukuru Mungu kwa baraka zake na nguvu ya mashabiki wake amefikia
hapo. Hiyo ni gari aina ya Range Rover Evoque. Gari hizi mara nyingi
hapa Tanzania kuna wakala wake kampuni inaitwa CMC Moters, ni moja kati
ya magari latest sana,” amesema Gadner.
Gadner
amezitaja sababu za mafanikio ya Jaydee ni pamoja na ‘karama na fadhila
ya mwenyezi Mungu, nguvu anayoipata kutoka kw mashabiki wa muziki
nchini.
“Wamekuwa
wakimwamini, wamekuwa wakimsupport na kwa jinsi hiyo ndio maana amekuwa
anapata mafanikio. Sababu ya tatu ni ile commitment yak wake yeye
mwenye kama msanii. Jaydee ni mtu ambaye ana bidii sana kwenye kazi yake
na anapenda sana muziki. Jambo hili linafanya siku zote awe makini na
umakini ule unampelekea awe na mafanikio kusema ukweli. Kitu kingine ni
kwamba ni mtu ambaye anathamini kesho yaani kama leo tumefanya vizuri,
je kesho itakuaje! Huwa anafikiria sana kutowaangusha mashabiki wa
muziki wanaomsupport.”
Gadner
amesema pamoja na kuwa na biashara yake ya Nyumbani Lounge, Lady Jaydee
anatarajia kuongeza zaidi miradi mingine. “Huyu bado ni mjasiriamali
mchanga anayejifunza zaidi na angependa kufanya biashara nyingi lakini
muda ni mdogo. Isipokuwa kwa mwaka huu alitarajia kufanya kitu kingine
kuongeza kama biashara. Hajawa tayari kusema ni kitu gani lakini
mwenyezi Mungu akijaalia heri na afya mwaka huu kuna biashara nyingine
Jaydee ataitambulisha, ukiacha Nyumbani Lounge na muziki,” Gadner
amefafanua.
Akiongelea
ushiriki wa Jaydee kwenye kipindi cha Coke Studio Africa, Gadner
amesema Jide amejiongezea connection kubwa na amejifunza mengi.
“Pamoja
na kuestablish mawasiliano lakini kumekuwa na kujifunza kwa malegend
kama Salif Keita na zaidi ya hapo kumekuwa na kama aina flani ya miradi
ya kufanya kazi pamoja na wasanii waliofika pale. Mzee Salif Keita
amemkubalia Jaydee wakati wowote atakapokuwa tayari aende Mali wakafanye
wimbo pamoja. Hali kadhalika Octopizzo kutoka Kenya tayari wameweka
kwenye line wimbo wa kufanya pamoja na Jaydee na wasanii wengine wa
Nigeria akiwemo Waje.
Gadner
amesema kwakuwa kufanya kazi na wasanii wa nje kunahitaji maandalizi ya
kutosha, muda muafaka ukifika Jaydee ataanza kuifutilia miradi hiyo.
Gadner
ambaye ni mtangazaji wa Times FM, ameongeza kuwa kwa mwaka 2014 Lady
Jaydee atasikika kwenye kazi alizoshirikishwa ukiwemo wimbo wa Juma
Nature, One, Songa na Nikki Mbishi, huku pia yeye akiachia wimbo mpya
uliotayarishwa na Bob Junior na kwamba Historia unaopatikana kwenye
Nothing But The Truth ni wimbo wa mwisho kutoka kwenye album hiyo.
Amesema video ya Historia imefanywa na kampuni ya Ogopa na kwa sasa ipo kwenye hatua ya editing.
Kuhusu wimbo mpya, Gadner amesema video yake itaongozwa na muongozaji Mtanzania aishiye Marekani, Hefemi.
“Nafikiri Jaydee alikuwa anataka afanye kitu cha tofauti na ndio maana akaamua amchukue director ambaye yuko nje ya Tanzania ili atupe picha na idea tofauti.”
“Nafikiri Jaydee alikuwa anataka afanye kitu cha tofauti na ndio maana akaamua amchukue director ambaye yuko nje ya Tanzania ili atupe picha na idea tofauti.”
No comments:
Post a Comment