.walimvua nguo na kumtupa kwenye ngome ya Mbwa wenye njaa 120
.Rais Kim Jong Un alikataa mjomba wake kunyongwa bali kuliwa na mbwa akiwa uchi wa mnyama
.kiongozi huyo na viongozi wengine 300 walishuhudia ukatili huo wa kutisha
.Adhabu hiyo iitwayo ‘Quan jue’ ilidumu kwa saa moja
.Mjomba wake alishtakiwa kwa hila na rushwa na matumizi mabaya ya madaraka
Na Damas Makangale, kwa Msaada wa Mtandao
Taarifa
zilizovuja kutoka mashirika mbalimbali ya habari duniani ni kwamba
Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un alishuhudia jinsi mjomba wake
Jang Thaek akiliwa na mbwa karibu 120 akiwa uchi wa mnyama kama adhabu
mbadala badala ya kunyongwa.
Taarifa
zinasema kuwa kiongozi huyo wa Korea Kaskazini aliamuru mjomba wake
avuliwe nguo zote na kubaki uchi wa mnyama na kisha mbwa kumtafuna akiwa
hai mpaka kifo chake, watetezi wa haki za binadamu wanasema ni adhabu
ya kikatili ambayo dunia haijawahi kushuhudia kwa miongo kadhaa.
Watu
wa karibu na wanafamilia wanasema Mjomba wake huyo alipelekwa kwenye
ngome hiyo na wasaidizi wake watano na kuachiwa kwa mbwa wenye njaa ya
siku tatu ili waweze kumshughulikia.
Mmoja
wa Mbwa Mwitu aliyekaa na njaa kwa siku tatu ambaye alitekeleza hukumu
ya Jang Song-Thaek mjomba wa Rais wa Korea ya Kaskazini.
Maelezo
ya kutisha yaliojitokeza katika ripoti katika gazeti la Straits Times
la Singapore , ambayo lilisema kitendo hicho ni cha kutisha na
kinajulikana kama ‘ Quan jue ‘, au ‘ utekelezaji wa adhabu kwa kutumia
mbwa wenye njaa.
Thaek
, alivaa suti ya bluu na pingu akisindikizwa katika mahakama ya Desemba
12, aliuawa na mbwa mwitu , kulingana na ripoti kutoka China.
Thaek
, alivaa suti ya bluu na pingu akisindikizwa katika mahakama ya Desemba
12, aliuawa na mbwa mwitu , kulingana na ripoti kutoka China.
Taarifa
zinaongeza kiongozi huyo wa Korea ya Kaskazini Kim Jong- Un alikuwa
anatoa ujumbe katika sikukuu ya mwaka mpya kwa wakorea wote nchini humo.
Wachambuzi
wanasema kiongozi huyo jeuri alikuwa na ujumbe maalum kwa viongozi
walioalikwa kwenye sherehe ya kifo cha mjomba wake kama onyo kwamba
wanapaswa kufuata taratibu na endapo kiongozi yeyote atakiuka taratibu
adhabu kali itachukuliwa dhidi yake.
Kim Jong-Un akiwa na mjomba wake enzi za uhai wake.
Kim Jong-Un, akitoa hotuba kwa taifa hilo siku ya sikukuu ya mwaka mpya.
Baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wa Korea ya Kaskazini ambao walishuhudia adhabu hiyo ya kikatili.
No comments:
Post a Comment