KOCHA Luc Eymael ambaye tayari ameshafanya mazungumzo ya awali
na viongozi wa Yanga, ameuambia uongozi wa klabu hiyo kuwa anaijua
vizuri Klabu ya Al-Ahly ya Misri na endapo watampatia kibarua hicho,
atawasaidia kuwang’oa katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Akizungumza na Mwanaspoti kwa njia ya mtandao,
Eymael ambaye ni raia wa Ubelgiji, alisema amefanya mazungumzo ya awali
na mmoja wa viongozi wa Yanga kupitia baruapepe, ambapo
alisema kama klabu hiyo itampatia ajira hiyo hana wasiwasi na uwezo wake katika kuwang’oa Al-Ahly ambao Yanga inatarajia kukutana nao raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
alisema kama klabu hiyo itampatia ajira hiyo hana wasiwasi na uwezo wake katika kuwang’oa Al-Ahly ambao Yanga inatarajia kukutana nao raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Yanga itaanza michuano hiyo dhidi ya timu ya
Comoronize ya Visiwa vya Comoro inayotajwa kuwa ni dhaifu na baada ya
hapo itakuwa na kibarua kizito dhidi ya wababe hao wa Misri.
Eymael aliyezaliwa miaka 54 iliyopita katika mji
mdogo wa Tongeren, Ubelgiji alisema hajajua Yanga inaundwa na nyota
wenye uwezo kiasi gani lakini anachoweza kuwaambia viongozi wa klabu
hiyo ni kwamba anazijua timu nyingi hasa Wamisri hao ambao tayari
wameshapata pigo kubwa kwa kuondokewa na nyota wao wawili muhimu akiwemo
mkongwe Mohamed Aboutrika aliyetangaza kutundika daluga Desemba mwaka
jana.
Eymael alisema tayari mezani kwake amepokea ofa
mbili kutoka klabu zinazoshiriki Ligi Kuu Algeria za CS Constantine na
CR Belouizdad na amepanga kuzitupilia mbali kama Yanga watachangamka
kuharakisha mazungumzo naye ya kumpa nafasi iliyoachwa na Ernest
Brandts.
Alisema kama Yanga watakuwa na nia ya kweli katika
kumpa kibarua hicho anawapa mpaka mwisho wa wiki hii na kama
hawatamtafuta katika muda huo ataingia katika mazungumzo ya kujiunga na
Costantine ambayo inamtafuta kila wakati kupitia mwenyekiti wa klabu
hiyo.
CS Constantine inashika nafasi ya nne ikiwa na
pointi 48, katika ligi inayoongozwa na ES Setif yenye pointi 59, wakati
Belouizdad inashika nafasi ya sita ikiwa na pointi 41, ambapo klabu zote
zinamwinda Mbelgiji huyo.
“Nilivyofuatilia Yanga ni timu nzuri, unajua
nilikuwa Kenya na AFC Leopards na hadi sasa wananihitaji, sijui uwezo wa
wachezaji wa Yanga na kuhusu akili zao na mbinu lakini kama watakuwa na
ubora hakuna shida katika kushindana na hao Al Ahly,” alisema Eymael.
“Kama Yanga wana nia ya kweli waambie wanitafute
mpaka kufikia mwisho wa wiki hii, wakichelewa baada ya muda huo
nitaingia katika mazungumzo na hawa Constantine ambao wapo katika nafasi
ya tatu kwenye ligi ya Algeria.
Bobby Williamson
Huenda mambo yakamnyookea Eymael kwa kuwa mpango
wa Yanga kumpa ajira Bobby Williamson, kocha wa Gor Mahia umegonga
mwamba baada ya kocha huyo kugoma kuja Tanzania na kubaki Kenya ingawa
viongozi wa Yanga wamedai kuwa hawakati tamaa hadi kieleweke.
Akizungumza na Mwanaspoti Bobby raia wa Scotland,
alisema amezungumza na mwenyekiti wa Gor Mahia mara baada ya kusikia
Yanga wanamhitaji.
No comments:
Post a Comment