Wengi wanafahamu kwamba mwanamke akipata mimba hawezi kuziona siku zake
za hedhi bila kujua kuwa ziko sababu nyingine zinazoweza kusababisha
jambo hilo.
Kwa kawaida mwanamke huacha kupata hedhi kitaalam huitwa Menopause
anapofikisha umri wa miaka 42 -55 na kuendelea.
Leo
tutazieleza sababu nje ya utaratibu huo wa kimaumbile unaoweza kumfanya
mwanamke asipate hedhi na moja kubwa ni tabia ya maisha yake ya kila
siku, yaani vyakula anavyokula (life
style).
SIGARA
Tatizo moja kubwa ambalo huwakumba wanawake wanaovuta sigara ni kukosa
hedhi au kuharakisha kutopata hedhi miaka miwili kabla ya wakati au umri
wa miili yao kufanya hivyo.
UNENE
Wanawake wengine hukumbwa na tatizo hilo kutokana na kuongezeka uzito.
Imethibitika kuwa uzito ukiwa mkubwa kwa wanawake unasababisha kuingia
katika hatua za kuacha kupata hedhi kwa kuchelewa kwa mwaka mmoja zaidi
ikilinganishwa na wanawake ambao hawana uzito mkubwa.Kitaalam hali hiyo
inatokana na uingilianaji wa mafuta (kwa watu wanene au walio na uzito
uliopitiliza) na homoni za kujamiiana yaani Sex homones.
ULEVI
Wanawake walevi wa pombe yaani wanaokunywa pombe kila siku nao wapo
kwenye hatari ya kukumbwa na tatizo hili.
Lakini walio katika hatari zaidi ni wale wenye umri kati ya miaka 25 na
49, hawa wanaweza kufunga hedhi kama wataendelea na tabia hiyo ya
unywaji wa pombe kila siku.
KUTOKULA NYAMA
Wengine ni wanawake ambao wanafanya mazoezi mazito mara kwa mara na
wenye umri kati ya miaka 39 na 49 au wasiokula nyama au vyakula
vinavyotokana na nyama (vegetarian) nao wamo katika hatari ya kukosa
kuona siku zao za hedhi.
Wengi wa wanawake wanaopatwa na tatizo hili hukumbwa pia na tatizo la
kuchelewa kuacha kupata hedhi kama inavyotakiwa wakiwa katika umri
unaotakiwa na hali hiyo huwahatarisha kwani wanaweza kukumbwa na hatari
ya kupata saratani ya matiti.
Menopause kama tulivyoeleza hapo juu, ni hatua ya kuacha kupata hedhi
ambayo hutokea wakati mwanamke akiwa na umri wa miaka 42-55 na
huambatana na usitishwaji wa kutolewa kwa mayai ya uzazi, kupungua kwa
kiwango cha homoni za kujamiiana, hivyo kusababisha kupungua kwa hamu ya
kujamiiana kwa mwanamke.
Hali hiyo husababisha tupu za mwanamke kuwa kavu, nywele kuwa nyembamba,
matatizo wakati wa kulala, matiti kusinyaa na kupata hedhi bila
mpangilio kabla ya kuacha kupata hedhi kabisa.
USHAURI
Mwanamke yeyote ambaye ataona dalili au kutopata hedhi yake muda muafaka
ni vyema akaenda kumuona daktari ili afanyiwe uchunguzi na kama
ataonekana ana tatizo la kiafya litapatiwa ufumbuzi. Wale wenye
matatizo ya tumbo wamuone mtaalam.
No comments:
Post a Comment