21 December 2013

WANAWAKE 11 WAFIKISHWA KORTINI PAMOJA NA WA SWEDEN KWA KUTUHUMIWA KURIKODI MKANDA WA NGONO NA MBWA!!

WANAWAKE 11 raia wa Kenya pamoja na Mzungu raia wa Sweden, hivi karibuni wamefikishwa katika mahakama moja iliyopo Mombasa kwa kudaiwa kunaswa wakirekodi mkanda wa ngono na mbwa.
Wanawake hao wakiwa kizimbani.
Wanawake hao waliotajwa kwa majina ya Beatrice Mueni Mwosa, Waithera Karanja, Marry Nyambura Kimani, Magdaline Wairimu, Celestine Nekesa, Dorcus Melisa, Ludia Nyaboke, Phidelia Mawia, Anne Wanjiku, Cecilia Nzambi na wengineo wanadaiwa kunaswa na polisi katika eneo la Nyali wakifanya uchafu huo.
Mzungu ambaye ni raia wa Sweden aliyeratibu mpango huo.
Imedaiwa mahakamani hapo kuwa katika eneo hilo, ilikutwa kamera na kompyuta mpakato ‘laptop’ mali ya Mzungu huyo anayedaiwa kuratibu mpango mzima, vitu ambavyo vilichukuliwa na polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Katika hatua nyingine, imedaiwa kuwa mwanaume huyo Msweden aliingia nchini humo kama mtalii na akawa karibu sana na mwanamke Mkenya ambaye inadaiwa ndiye aliyewakusanya wanawake wengine kwa ajili ya kukamilisha zoezi hilo.
Hata hivyo, upande wa mashitaka utakuwa na kazi kubwa ya kuthibitisha kama kweli wanawake hao wamehusika kwani inadaiwa wakati wanakamatwa, mmoja tu ndiye aliyekuwa amesharekodi ‘scene’ yake.
...Wakitoka mahakamani.
SERIKALI YA KENYA YACHARUKA
Wakati kesi ikiendelea mahakamani, makamu wa rais wa nchi hiyo, William Ruto ameeleza kusikitishwa na tukio hilo, akasema amewaagiza watu wa usalama kuhakikisha raia wa kigeni wenye tabia chafu kama hizo wanatimuliwa mara moja.
“Nimewaambia watu wa Internal Security (Usalama wa Ndani) kwamba watu kama hawa hawafai kuwa katika taifa letu la Kenya, wapandishwe ndege waende kwao,” alisema Ruto.
...Baadhi yao wakiwa wamejiinamia kwa aibu.
WABONGO WAONYWA
Kufuatia tukio hilo, mademu Bongo wenye uhusiano wa kimapenzi na Wazungu wametakiwa kuwa makini kwani baadhi si watu wema.
Wakizungumza na Risasi Mchanganyiko baada ya kesi hiyo kuwa gumzo, baadhi ya watu wamesema kilichotokea Kenya ni fundisho kwa wasichana wa Kibongo wanaoshobokea Wazungu.
...Mmoja wao huyu hapa.
“Hilo limetokea Kenya lakini ni fundisho kwa mabinti wetu hapa nchini ambao wanakimbilia kuanzisha uhusiano na Wazungu.
“Kuna uwezakano wapo wanaofanyiwa vitendo hivyo kwa kuahidiwa pesa nyingi au kuwekewa mitego na hatimaye kurekodiwa picha chafu wakiwa wanajua au hawajui,” alisema mama Salma wa Magomeni jijini Dar aliyedai kwamba amekuwa akifuatilia kesi hiyo tangu ilipoanza kusikilizwa.
CREDIT-GPL

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname