Dunia haiishi mambo na vijimambo, bibi na bwana harusi
waliojikita katika kutetea haki za kupiga picha uchi, Gypsy Taub na
mkewe Jaymz Smith waishio San Francisco wamejikuta wakilia honeymoon yao
lupango baada ya kuchojoa nguo zao zote wakati wakifunga ndoa.
Kwa mujibu wa ‘The San Francisco Chronicle, bibi harusi alifika
katika eneo la tukio akiwa amevaa nguo kama kawaida lakini alizichojoa
zote ghafla na kubaki mtupu kama alivyozaliwa kisha akapaza sauti, “hii
ni kwa ajili ya kupinga sheria zanazokataza kuwa mtupu kwa namna ambayo
imekuwa katika ndoa.”
Naye mfungishaji ndoa ambaye sio kiongozi wa dini yeyote, alisema
“najua watu wa San Francisco wako nyuma yangu,” na kisha kuwaambia wana
ndoa hao, “sasa mnaweza ku-kiss na kufanya ngono.”
Gazeti hilo limeripoti kuwa tukio hilo lilifanyika hadharani karibu
na makazi ya watu ambapo wanawake wengi na watoto walikuwa wakipita eneo
hilo.
Baada ya shangwe za ndoa hiyo, maharusi walichukuliwa na gari la
polisi na kupelekwa panapohusika, na ripoti zinasema walifunguliwa
mashitaka kwa kosa la kujiachia watupu hadharani.
Hata hivyo wawili hao waliachiwa baadae huku tarehe za honeymoon zikiwa zimeishia selo.
Lakini waliporudi uraiani waliliambia The San Francisco Chronicle kuwa ndoa yao ilikuwa nzuri na ya kufurahisha.
“It was fantastic…it surpassed all my expectations. It was just an awesome party.” Bwana harusi Taub alijigamba.
No comments:
Post a Comment