28 December 2013

Video ya mtoto wa ‘kizungu’ aliejaribu kurap wimbo wa Young Killer

Hii itakua sio mara ya kwanza kwa millardayo.com kuripoti stori ya ‘Wazungu’ kupenda au kuongelea nyimbo ambazo zimefanywa na Wasanii wa Kitanzania ambapo Marlow alishawahi kuchukua headlines kwa single yake ya ‘pipi’
Time hii imemuangukia Young Killer, mkali kutoka Mwanza ambae uzito wa jina lake umeongezeka kupitia shindano la Super Nyota ambalo hufanyika likiambatana na Tamasha la Fiesta ambalo hufanyika kila mwaka kwenye maeneo mbalimbali ya Tanzania.
Mtoto huyu wa ‘kizungu’ alieonyesha mapenzi yake kwa single ya ‘Mrs Super star’ ni raia wa Marekani na kwenye hii video amesema alikua hamjui Young Killer lakini baada ya kuambiwa kuhusu kilichoimbwa kwenye wimbo wa ‘Mrs Super star’ akawa amemkubali na kujiunga kwenye mstari wa mashabiki wake, anasema Killer angekua Marekani angetengeneza pesa nyingi. source- millardayo

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname