BONDIA
Floyd Mayweather amefufua vita ya maneno na mpinzani wake, Manny
Pacquiao pamoja na kuwakandia pia Amir Khan na Marcos Maidana kwa staili
ile ile. Pamoja na kumuita Pacquiao majeruhi wa Juan (Manuel) Marquez
akikumbushia kipigo cha Mfilipino huyo mwishoni mwa mwaka 2012 kwa
Knockout (KO) kutoka kwa Mmexico huyo, Mayweather ameweka picha ya
'kubumba' akiwa amemsukumia konde zito usoni. "Sasa unaniambia nakwenda
kula makombo ya Juan Marquez? Acha nizungumze na IRS juu ya hili,"
alitweet mbabe huyo.Hizi ni salamu: Floyd Mayweather (kushoto)
akimsukumia konde Manny Pacquiao, kuashiria pambano baina yao linaweza
kuokea Awali iliripotiwa, Khan anajiandaa kuwa mpinzani ajaye wa
Mayweather mwezi Mei, lakini Mmarekani huyo ameendelea kuwaambia
mashabiki wake kwamba ataendeleza ubabe wake.Kama ambayo wengi
wanchukulia Khan atakuwa mpinzani dhaifu kwa Mayweather, bondia huyo
naye amembeza akimuita 'Con Artist' katika picha ambayo amebandika ya
kubumba akimchapa konde hadi kuelekea sakafuni. Amesema: "Hebu fikiria,
nini Amir "Con Artist" atapata kama atachaguliwa kuingia anga za
Mayweather,". Mtu mwingine anayechukuliwa kama mpinzani wa baadaye wa
bondia huyo bingwa wa madaraja matano ya uzito duniani ambaye hajawahi
kupigwa ni Muargentina, Maidana, kufuatia ushindi wake wa kushitua dhidi
ya mbabe aliyepewa jina 'New Mayweather', Adrien Broner. >Akiwa
amebandika picha kama hizo,akimtandika ngumi ya mkono wa kulia,
Mayweather pia ametweet kuhusu bondia huyo: "Naweza kuagiza kipande
kimoja na biskuti tafadhali? Hakuna sehemu."
Sakafuni: Floyd Mayweather ameweka picha akimuadhibu Muingereza Amir Khan, pambano lao linatarajiwa kufanyika Mei
Konde la nguvu: Lakini Floyd Mayweather anajiamini pia atampiga Marcos Maidana (kushoto)
Mfalme wa masumbwi: Floyd Mayweather amekuwa akipewa heshima ya bondia bora kwa muda mrefu
No comments:
Post a Comment