Huku akikataa
kuweka bayana nia yake ya kuwania urais kwa maelezo kwamba muda wa
kufanya hivyo haujawadia, Makamba aliwaambia viongozi hao wa dini kwamba
wagombea hao wanapopita wawasomee sifa za uongozi katika Biblia na
kusema kumekuwapo mjadala wa sifa za uongozi kuhusu kijana na kusema
amekuwa akitoa mwito kwa vijana wasiokuwa na makandokando kushiriki na
kujitokeza katika kusaidia nchi ipone.
Akizungumza juzi
usiku mjini hapa katika chakula cha pamoja na maaskofu na wachungaji
kutoka Umoja wa Makanisa ya Kikristo wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa, Makamba
ambaye pia ni mbunge wa Bumbuli (CCM), alisema: “Huu ni wakati wa kila
mmoja kutafakari hatima ya nchi yetu. Ndugu zangu… nadhani tuzungumze
machache yanayohusu nchi yetu na Taifa letu, kwa sababu sote ni
Watanzania na wote tuna hamu ya kujua na kutafakari mustakabali wa nchi
yetu, umoja wetu, amani yetu na utulivu wetu.”
Alisema vijana
wengi wamekuwa waoga kwa madai kwamba hawana fedha, uzoefu lakini
akasema maaskofu na wachungaji wanapaswa kuwa mashahidi kupitia vitabu
kwani katika Yeremia imeelezwa jinsi Mungu alivyompatia unabii Yeremia
ambaye alidai yeye bado mdogo.
“Yeremia alipopewa
unabii alilalamika mimi mdogo mimi siwezi, lakini Mungu alimwambiaje,
ngoja nisome, (Yeremia 1: 4-10) …. Kabla sijakuumba ndani ya tumbo la
mama yako nilikujua, kabla hujazaliwa nilikutenga kwa kazi maalumu,
nilikuweka uwe nabii kwa mataifa,” alisema na kuongeza:
“Bwana alimwambia
usiseme, mimi ni mtoto mdogo. Utakwenda popote nitakapokutuma na kunena
lolote nitakalokuagiza, usiwaogope, kwa maana niko pamoja nawe
nikuokoe.”
Alisema Tanzania
inapita katika kipindi kigumu, hivyo viongozi wa dini wanapaswa kuongoza
maombi yatakayoiwezesha kupata kiongozi mwenye sifa ya kuivusha katika
kipindi hicho.
Makamba amesema
nchi inakabiliwa na nyufa kama vile rushwa, udini, ukabila, Uzanzibari
na Uzanzibara, huku akirejea hotuba ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu
Julius Nyerere ya Machi 1995, ambayo aliyataja mambo hayo kuwa nyufa
zinazoweza kuliangamiza taifa.
Alisema Tanzania
inahitaji uponyaji na ikibidi kuanza upya kwa maana ya aina ya uongozi
unaohitajika hivi sasa na kwamba ili kutimiza lengo hilo, viongozi wa
dini wana nafasi kubwa ya kutafakari na kuielekeza nchi njia sahihi ya
kufuata.
“Shughuli za siasa
zimeingiliwa na matapeli, lakini hata shughuli yenu pia imeingiliwa na
matapeli. Sasa tunapotafuta uponywaji wa nchi yetu ninyi mna nafasi
kubwa kwani uponyaji tunaouzungumzia ni wa maovu ya kiroho, uongo,
ubakaji na vitu kama hivyo, ninyi mna nafasi kubwa sana,” alisema.
Alisema viongozi wa kisiasa pia wanayo nafasi yao katika kuponya taifa lakini lazima wanapofanya kazi hiyo wawe wasafi.
Alisema askofu au
mchungaji akihubiri anapaswa kuwa msafi na hata katika uongozi wa siasa
anaposimama mtu na kusema yeye ni jawabu la matatizo ya wananchi ni
vizuri kumtazama sura yake kama ameacha (maovu).
“Tunapoomba uongozi
wa kisiasa zipo sifa kwani tunaomba kuongoza watu wa Mungu ambao ni
walewale wanaokuja kanisani ndiyo wanaokuja katika siasa, kuongoza watu
wa Mungu siyo kitu kidogo…… hivyo lazima vigezo vya kuongoza watu hawa
viwe vikubwa sana,” alisema
Rasilimali za nchi
Alisema Tanzania
hivi sasa inakabiliwa na changamoto zinazoweza kuitwa kuwa ni za kidunia
na za kibinadamu zinazojumuisha masuala kama vile upatikanaji wa huduma
za afya, maji na elimu.
“Tunagawanyika
ingawa migawanyiko hiyo si ya kidini, rangi na kikabila... iko ya namna
gani, watu wachache wananufaika na keki (rasilimali) ya taifa kuliko
wengine,” alisema Makamba na kuongeza:
“Sasa Serikali,
hili kwetu ni muhimu sana…. hakuna kitu muhimu kama kuendelea kujenga
umoja wa taifa letu, migawanyiko hii ndiyo changamoto. Elimu anayoipata
mtoto wangu ndiyo anaipata mtoto wa Rwamgasa, Kwimba na Nyarugusu?”
Alisema usawa
katika elimu pamoja na huduma nyingine kama afya na nyingine muhimu,
ndiyo msingi wa ujenzi wa taifa lenye amani na umoja kwani kila mmoja
atajihisi kunufaika na rasilimali za nchi.
Naibu Waziri huyo
alisema changamoto nyingine zinazoikabili nchi ni vitendo vya rushwa,
ubadhirifu na wizi wa mali ya umma, ubakaji, utapeli na kuporomoka kwa
maadili.
Alisema taifa
halipaswi kusubiri adhabu kutoka kwa Mungu kama inavyosomeka katika
vitabu vitakatifu ambako kuna ushahidi kuhusu gharika wakati wa Nuhu,
pia moto wakati wa Sodoma na Gomora, huku akiwapa changamoto viongozi wa
dini kukabiliana uovu unaoshika kasi.
“Sasa taifa letu
lina miaka 52 ya Uhuru wa Tanganyika na mwakani tunaadhimisha miaka 50
ya Uhuru wa Zanzibar. Miaka 50 ni mingi kwa binadamu, lakini ukweli ni
kwamba kazi ya kulijenga taifa letu ndiyo inaanza.”
Shinikizo la maaskofu
Baada ya hotuba
yake, baadhi ya maaskofu na wachungaji walisikika wakimshinikiza Makamba
atangaze nia ya kugombea urais lakini alisema atafanya hivyo wakati
mwafaka ukiwadia.
Mwenyekiti wa Umoja
wa Makanisa hayo ya Kikristo, Askofu Charles Sekelwa alisema: “Viongozi
wa dini tukubaliane kuwa walezi na tusimkatae mtu kwa dini yake wala
kabila lake. Wakijitokeza vijana huko mbele tuwaunge mkono, hayo maneno
ni ya mtu mwenye hekima”.
Askofu
Jacob Lutabija alisema amepokea ujumbe mzito ambao atakwenda kuutangaza
kwa waumini wake wa Musoma akisema kwa watu wenye hekima zao wametambua
nini wanapaswa kufan
CREDIT -Mwananchi
No comments:
Post a Comment