Naibu
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwigulu Nchemba, amemwonya
Spika wa Bunge, Anne Makinda kuacha kutumia vibaya fedha za Serikali kwa
kuwapa posho wabunge kwa ajili ya kwenda kwenye michezo nje ya nchi.
Nchemba
ambaye ni Mbunge wa Iramba Magharibi alitoa kauli hiyo jana bungeni
wakati akichangia Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ushuru
wa bidhaa ya mwaka 2013 iliyowasilishwa na Naibu Waziri wa Fedha, Saada
Mkuya Salumu.
Mkuya
katika maelezo yake alisema kuwa kodi hiyo imefutwa kwa laini za simu
kwa mtu mmoja mmoja na badala yake imeongezwa katika kodi kutoka
asilimia 14.5 hadi asilimia 17.
Katika
mchango wake, mbunge huyo alionya kuwa kumekuwa na tabia ya kutumia
vibaya fedha za umma jambo alilosema linaanzia ndani ya bunge.
"Naomba
tukubaliane katika kubana matumizi, na hivyo ninakuomba Mheshimiwa Spika
tuanze na ofisi yako achana na kutoa fedha kwa kuwapa wabunge kwa ajili
ya kwenda Dubai kwa burudani,"alisema Nchemba.
Alisema
umefika wakati ambao Serikali inatakiwa kufanya uamuzi wa kutumia fedha
katika mambo muhimu ambayo yanaigusa jamii kuliko mambo ambayo hayana
maana. Kwa upande mwingine aliwalaumu watendaji kuwa wameiangusha
Serikali ya Chama Cha Mapinduzi kwa kushindwa kutoa ushauri na usimamizi
mzuri katika makusanyo ya kodi.
Kwa
upande wake Mbunge wa kuteuliwa James Mbatia aliinyooshea vidole
Serikali kuwa ndiyo iliyovuruga mchakato mzima wa makusanyo ya kodi
ambayo muswada wake ulishapitishwa.
Mbatia alitoa sababu kuwa ndani ya Serikali wamekuwa wakiamua mambo lakini kwenye utekelezaji wake wanagawanyika.
Chanzo:Mwananchi
No comments:
Post a Comment