Mwanamuziki mrembo wa Kenya na hitmaker wa Kitu Kimoja,
Avril Nyambura, amesema yeye na mchumba wake raia wa Afrika Kusini wapo
kwenye mazungumzo ya ndoa yao japo amesema hawataki kuharakisha.
“Tumefahamiana kitambo sasa na tunafurahia maendeleo mapya.
Tunajadili masuala yanayohusiana na ndoa lakini hatuna pressure kabisa
ya kuharakisha mchakato,” mrembo huyo aliuambia mtandao wa Standard
Media.
“Harusi haiwezi kuwa mapema. Yeye ni Mzulu mimi ni Mkikuyu na kuna masuala ya kiutamaduni kwenye mchakato mzima.”
No comments:
Post a Comment