NYOTA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper amefunguka kuwa filamu yake
aliyoitoa kumuenzi marehemu Steven Kanumba iitwayo After Death
ilimlostisha kwa kuwa ilimpatia hasara kubwa.
Jacqueline Wolper.
“Nilitengeneza ile filamu kwa hela nyingi kidogo, kama milioni 35 au 40,
nikafanya na uzinduzi pale Leaders Club uliogharimu kama milioni 13
hivi, lakini nilipokwenda kwa Wahindi wakanipa shilingi milioni 25,
yaani inakatisha sana tamaa,” alisema muigizaji huyo wakati alipofanya
mahojiano maalum na waandishi wetu.
Credit: GPL
No comments:
Post a Comment