Hivi karibuni hapa jiji
mwanza mkazi mmoja wa Igoma Aliefahamika kwa jina moja la Consolata
amepigwa na mmewe na kung’atwa sikio na mtu anaedaiwa kuwa ni hawara wa
mumewe bi consolata amesema alikuwa akigombana na mumewe ndipo hawara
yake huyu alipokuja na kusema ngoja tukuonyeshe maana hutujui ndipo
alipong’atwa sikio na kuondolewa sikio zima
Mara baada ya kufanyiwa
ukatili huo alienda kulipoti katika kituo cha polisi lakini kwa madai
yake ni kwamba watuhumiwa waliachiwa huru kwa kuwa walikuwa wakijuana na
baadhi ya askari waliokuwepo kituoni .Ndipo bi consolata alipochukua
hatua za kutafuta wasamalia wema kama waandishi ili waweze kumsaidia
aweze kupatiwa matibabu kwani ni mgeni jiji mwanza toka kigoma na
alikuja mwanza kwa ajili ya kumsalimu mumewe.
Baada ya kuzungumza na
waandishi alipelekwa kwenye taasisi ya kivulini ambao mpaka sasa
wanampatia huduma ya matibabu ukatili huu kiukweli ni aibu kubwa kwa
taifa letu
No comments:
Post a Comment