Staa wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper amefunguka kuwa suala la yeye
kuachana na aliyekuwa mpenzi wake, Abdallah Mtoro ‘Dallas’
halikusababishwa na ukata kwani yeye hakufuata fedha kwa mwanaume huyo.
Akijibu swali la paparazi wetu lililomtaka afunguke kama alifuata
mkwanja kwa Dallas, Wolper alisema moyo wake huwa hauna tamaa ya fedha
na aliingia katika penzi la Dallas kwa mapenzi aliyokuwa nayo wakati huo
na kwa kuwa yaliisha, maisha yanaendelea.
“Sikufuata pesa kwa Dallas, pesa ni pesa na mapenzi ni mapenzi. Kama ni
pesa nilikuwa nazo na hata kabla sijawa naye na sasa pia ninazo,
waniache,” alisema Wolper.
No comments:
Post a Comment