14 November 2013

HATIMAYE..!Waliomlawiti mwanafunzi kwa agizo la Mwalimu wakamatwa na Polisi

Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro limewakamata watu  watatu kwa kosa la kufanya kitendo cha kinyama cha kulawiti mwanafunzi mmoja wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Nyerere iliyoko kijiji cha Lembeni wilayani Mwanga. 

Akithibitisha hayo kamanda wa polisi mkoani hapa Robart Boaz amesema tukio hilo lilitokea Novemba 03 mwaka huu majira ya saa kumi na mbili jioni katika kijiji cha Lembeni ambapo watuhumiwa hao walifanya kitendo hicho cha kinyama katika nyumba inayomilikiwa na Charles Natanaeli alimaarufu Nguto.
Kamanda Boaz amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Januari Alhaji(20) ambaye ni dereva wa magiri ya fuso na Patriki Salpisi(20) ambaye ni fundi wa magari pamoja na mwenyenyumba mwenyewe alimaarufu Nguto.

Amesema watuhumiwa hao walitumwa kufanya kitendo hicho na mwalimu mmoja wa shule hiyo ya sekondari Nyerere aliyetambulika kwa jina Hadija Juma.

Aidha Boaz amesema hakuna taarifa zozote zilizoripotiwa polisi kuhusiana na kijana huyo kutaka kufanya kitendo hicho na kuongeza kuwa mwalimu huyo alituma vijana hao kufanya kitendo hicho kwa ajili ya kulipiza kisasi ambapo inadaiwa huyo kijana alitaka kumbaka mtoto wa mwalimu huyo mwenye umri wa miaka mitatu.

Hata hivyo Boaz amemuagiza Mkuu wa polisi wilayani Mwanga kuhakikisha wanafuatilia kesi hiyo kwa ukaribu ili kuhakikisha watuhumiwa hao wanapata adhabu kali inayolingana na kosa hilo.

Mwanafunzi huyo alifikishwa katika hospitali ya Mwanga ambapo paka sasa yuko hapo kwa ajili ya kuwekewa ukaribu wa washauri na saa

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname