Mastaa wa filamu Bongo, Rose Ndauka na Wema Sepetu wanadaiwa kuingia
vitani, mpambe mmoja wa Wema akitumia mtandao wa kijamii wa Instagram
alimtuhumu Rose kwamba aliwahi kushiriki kikao kimoja kilichokuwa
kikimjadili ‘madam’ huyo sanjari na kumtukana.
Akizungumza na mimi kwa njia ya simu juzi kuhusiana na tuhuma hizo, Rose alisema anashangaa matusi anayotukanwa na mtu huyo kwani ana mwaka mmoja hajawahi kukanyaga katikia viwanja hivyo vilivyopo Kinondoni, Dar.
Rose Ndauka
“Kiukweli huyo mtu amenitukana bure, hajakaa na kufanyia uchunguzi hizo
taarifa alizopewa, mimi sikumbuki kama kuna siku niliwahi kukaa Leaders
na kuanza kumsema vibaya Wema kwani nina mwaka sijawahi kufika Leaders.“Binafsi sina muda huo wa kumzungumzia mtu au kukaa na mtu ambaye hana faida kwangu. Mimi rafiki yangu ni mchumba wangu (Malick Bandawe), mama yangu na ndugu zangu zaidi ya hapo tunakutana shutingi tukimaliza narudi kwangu, namsihi huyo mpambe wa Wema afanye tena uchunguzi,” alisema Rose.
Juzi,tulimsaka Wema kwa njia ya simu ya mkononi ili azungumzie madai hao lakini hakupatikana. Hata hivyo, habari zinasema kuwa mtu aliyemtukana Rose kwenye mtandao alitumwa na Wema au Wema mwenyewe.
Tangu Diamond kurudiana na Wema na kusambaza picha zao katika mitandao ya kijamii, hivi karibuni Wema kufiwa na baba yake mzazi (Isaac Sepetu) na baadhi ya wasanii wa Bongo Muvi kususia msiba huo, kumeibuka makundi ya watu kazi yao kubwa ni kutukana watu ambao wako tofauti na Wema
No comments:
Post a Comment