26 November 2013

WASANII WA BONGO MOVIE WASUSIA TENA KISOMO CHA MAREHEMU SHARO MILIONE KATIKA KUMBUKUMBU YA MWAKA MMOJA TANGU AFARIKI.!


Marehemu SHARO MILIONEA
 
Tarehe ya leo familia ya marehemu Sharo milione na watanzania wanamumbuka mwanamuziki huyo tangu alipotutoa mwaka jana tarehe kama hii.
 
Habari toka Mkoani Tanga zinasema kuwa wasanii mbalimbali wa kundi la Komedi wako mkoani humo kwa ajili kushiriki kisomo huku kukiwa na dosari kwa wasanii wa bongo movie ambao hakuna hata mmoja aliyetia maguu yake huko.
Mwandishi ambae yuko Mkoani humo kushiriki kikamilifu kwenye kumbukumbu hiyo alisema kuwa shughuri hiyo inaendelea vyema huku Kitale ndiye anaeongoza kisomo pamoja kusimamia shughuri nzima.
Hata hivyo mashabiki wengi wa filamu wamesikitishwa kwa ubaguzi unaoendelea kwa wasanii wa Bongo Muvi ambao hawataki kushirikiana na wenzao kwa madai kuwa wao ni bora kuliko wenzao

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname