Umati mkubwa uliokuwa ukimsindikiza Sheikh Shariff Mikidadi kutoka
viwanja vya Uyui Sekondari eneo ambalo lilikuwa likifanyika Kongamano la
dini ya kiislamu kuelekea nyumbani kwao Kiloleni manispaa ya Tabora
ulisababisha barabara kadhaa kufungwa kwa muda kutokana na wingi wa watu
katika msafara huo ambao wake kwa waume walikuwa wakimshangilia Sheikh
Shariff kwa kutaja jina la
MwenyeziMungu.Sheikh Shariff alijikuta akitokwa na machozi ya furaha kwa kuona namna watu wanavyomthamini na kumpenda pasipo kujali dini zao.
MwenyeziMungu.Sheikh Shariff alijikuta akitokwa na machozi ya furaha kwa kuona namna watu wanavyomthamini na kumpenda pasipo kujali dini zao.
Licha ya kuwa giza lilianza kuingia umati huu mkubwa wa watu waukujali
suala hilo na hivyo kuliona giza kama mchana kweupe, wakalazimika
kutembea kwa umbali mrefu kutoka katika viwanja vya Uyui Sekondari hadi
nyumbani kwao Sheikh Shariff. .
Watu wengi walihitaji kushikana mkono na Sheikh Shariff lakini haikuwa
rahisi kutokana na wingi wa watu,wapo waliobahatika kufanya hivyo na
kuamini kuwa wamepata neema ya pekee ya mkono wa baraka wa Sheikh
Shariff Mikidadi.
Awali Sheikh Shariff wakati akimalizia na kufunga Kongamano hilo la
mwaka 2013 hapa mkoani Tabora alisoma Dua maalumu kuwaombea watu wenye
shida na matatizo mbalimbali ambapo idadi kubwa ya watu walianza
kuanguka chini wakiwa wamepandisha mashetani jambo lililoshangaza wengi
katika Kongamano hilo lililofanyika kwa muda wa siku tatu.
Sheikh Shariff Mikidadi ambaye ni mzaliwa wa kata ya Kiloleni manispaa
ya Tabora alikuwa akitumia muda mwingi kuwaasa Waislamu kuwa na umoja
na mshikamano lakini kubwa zaidi ni kumcha MwenyeziMungu.
Mmoja kati ya viongozi wa dini ya Kiislam nchini Afrika Kusini Sheikh
Salim Dede ambaye anatokea taasisi ya kimataifa ya Islamic Propergation
Centre naye alikuwa ni miongoni mwa viongozi waliofikisha ujumbe katika
Kongamano hilo lililoandaliwa na taasisi ya SHEIKH SHARIFF MUSLIM
FOUNDATION ambalo litakuwa likifanyika kila mwaka nchini Tanzania na nje
ya Tanzania.
Umati mkubwa ukiwa umetulia kusikiliza mawaidha ya dini ya kiislamu katika Kongamano hilo.
Sheikh Shariff Mikidadi akiwa jukwaani akitoa mawaidha katika Kongamano
hilo lililofanyika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Uyui mjini Tabora.
Baadhi ya wanawake wa kiislamu walikusanyika kwa wingi katika Kongamano
No comments:
Post a Comment