Meya
anayejiita 'wa Mahakama' wa Manispaa ya Ilemela Henry Matata
amewaburuza TAKUKURU madiwani wanne wa CHADEMA, paparazi imebaini.
paparazi
limebaini madiwani hao, JOSEPHAT MANYERE , ROSE BROWN, GLADYS KIWIA na
LUCY KAZUNGU, wanatuhumiwa kupokea posho ya zaidi ya Sh milioni 3 bila
kusafiri.
Madiwani
hao wanatuhumiwa na Meya kwamba kila mmoja alipokea posho ya ya
shilingi 80,000/- kwa siku kumi kila mmoja kwa safari ya kwenda Mbeya
kikazi lakini hawakwenda.
Habari za uhakika zilizothibitishwa na maofisa wa Takukuru, Mwanza, taarifa imewasilishwa kwao jana.
Kwa
mujibu wa Meya huyo, madiwani hao wanastahili adhabu kwa mujibu wa
Sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 329 ya mwaka 2002.
Meya
huyo ambaye pia ni diwani wa kata ya Kitangiri alipata udiwani kwa
tiketi ya Chadema kabla ya kuvurugana na Chama chake na kamati kuu
kuamua kumtimua uanachama na yeye kukimbilia mahakamani kuzuia
kutimuliwa, kesi hiyo iko Mahakama kuu inaendelea kuunguruma.
Amekuwa
akijiita Meya wa Mahakama kwa kuwa Mahakama ndiyo ilizuia kufukuzwa
kwake na hivyo kumfanya aweze kugombea umeya ambao alishinda kwa kuungwa
mkono na CCM.
Matata
tayari ameshawafukuza udiwani madiwani wawili wa Chadema, Kahungu wa
kata ya Kirumba na Abubakari Kapera wa kata ya Nyamanoro kwa kushindwa
kuhudhuria vikao vitatu mfululizo wakati wakigomea vikao wakigoma
kumtambua yeye kama Meya.
Manyerere
ambaye ndiyo alikuwa Meya wa Jiji la Mwanza baada ya uchaguzi Mkuu wa
2010 kabla halijagawanywa kuzaa halmashauri ya Manispaa ya Ilemela na
Jiji la Mwanza lenyewe, aliondolewa katika kiti hicho kwa zengwe
lililoanzishwa na diwani wa Igoma kupitia Chadema Adam Chagulani, na
kuungwa mkono na Matata na madiwani we CCM na CUF.
Chagulani
alifukuzwa Chadema kufuatia kuanzisha hoja ya kutokuwa na Imani na Meya
wa Chama chake, yeye pia alifungua kesi mahakamani kupinga kuvuliwa
uanachama
No comments:
Post a Comment