15 November 2013

MAAJABU KATIKA MSIBA WA BABA YAKE BAHATI BUKUKU...KABURINI WAZIKA MGOMBA

Ni fedheha sana msibani!
MWIMBAJI maarufu wa nyimbo za Injili, Bahati Bukuku hivi karibuni alipatwa na simanzi kubwa baada ya aliyekuwa baba yake mdogo, Lwaga Bukuku kufariki dunia, lakini wakati kaburi likiwa limechimbwa Sinza Makaburini, iliamriwa msiba huo usafirishwe kwao Mbeya na hivyo kusababisha shimo hilo kuzikwa mgomba badala ya mwili wa mtu.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Novemba 7, mwaka huu, huko Tabata Kisukuru wakati waombolezaji waliojitokeza kwa wingi wakiwa wanatoa heshima za mwisho kwa marehemu ambaye alikuwa akazikwe kwenye Makaburi ya Sinza, jijini Dar es Salaam ambako tayari kaburi lake lilishachimbwa.

Lwaga, baba mdogo wa mwimbaji huyo ambaye muda wote wa kuumwa kwake alikuwa akiuguzwa naye, alifikwa na umauti Novemba 5, mwaka huu akiwa Hospitali ya Kadinary inayomilikiwa na Dk. Mvungi iliyopo Ukonga jijini Dar es Salaam na baada ya kifo chake, shughuli za msiba zilihamia nyumbani kwa Bahati Tabata Kisukuru.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname