Hata kama sio shabiki wa diamond ila
kuna kitu lazima uwe kinakuvutia kutoka kwake.Unaweza kujitahidi
kumchukia labda kutokana na skendo zake za nje ya muziki wake ila
ukirudi kwenye muziki wake nadhani anastahili kuwa pale alipo.
Kuanzia muonekane wake mpaka anavyoweza kuji-brand kimataifa na anavyojua kucheza na akili za mashabiki.
Wasanii wengi wa bongo flava wana tabia
ya kurithika kwa mafanikio yao ila Diamond toka atoke na Kamwambie mwaka
2009 mpaka 2013 amezidi kwenda juu bila kuonyesha kusuasua wala
kutetereka.
Angalia video ya number 1.Wimbo unaweza
sema ni wa kawaida kabisa ukilinganisha na mbagala, kamwambie au
nitarejea ila akili ya kwenda kufanya video cape town,south africa
kumeifanya nyimbo iwe number 1 kama jina lake lilivyo.
Ushawahi kujiuliza Ali kiba yupo wapi
pamoja na kuwa kila mtu anajua ni mkali kuliko diamond?Ali kiba toka
atoe my everything mwisho wa mwaka jana amepotea hata video
ajatoa.Tukaja kumuona kwenye kidela na Abdu kiba bila kurefusha maneno
Ali anashindwa kuufanya mziki wake kama mashabiki wake wanavyotarajia
labda pengine angekuwa anafukuzana na diamond ila matokeo yake vijana
wake kama Rich mavoko na Dimpoz ndio wapo nyuma ya Diamond huku Ali
akibaki msanii mkali ambae ameshindwa kuendelea kutuonyesha ukali wake
sijui anawaza nini!
Ushawahi kujiuliza kama ule wimbo wa
airtel hands across the world waliopiga wakina r.kelly,fall ipupa,2 face
kama nafac ile angeipata diamond leo angekuwa wapi?
Diamond leo anatuletea remix ya number 1
f.t Davido kila mtu anaisubiri kwa hamu ila Ali alishindwa hata
kutuletea remix ya Dushelele f.t Fally ipupa pamoja kukaa nae wiki nzima
wakifanya wimbo pamoja.
Diamond ni mjanja anaejua biashara ya
mziki ilivyo labda pengine ni management yake inayomsimamia.Diamond
kaweza kuubadilia mziki wetu kwa kiasi chake leo ndio msanii anaelipwa
pesa nyingi kwa show.
Nampenda ali kiba,naipenda sauti
yake,anajua mziki kuliko Diamond ila Ali ameshindwa kubadilika na
kukubali soko la mziki linataka nini.
Amka Ali huyu Diamond hakuwezi ila
usipokuwa makini utajikuta nyuma ya rich,barnaba,dimpoz na ben pol maana
mziki sio kuimba peke yake mziki ni biashara pia
No comments:
Post a Comment