MJUMBE wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba
ambaye pia ni Mhadhiri Mwandamzi wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Bagamayo
(UB), Dk. Sengondo Mvungi, usiku wa kuamkia leo amevamiwa na watu
wasiyojulikana na kukatwa mapanga maeneo mbalimbali mwilini ikiwemo
sehemu za kichwani kwa madai ya kutaka wapatie fedha. Watu hao
walitimiza lengo lao hilo baada ya Dk. Mvungi kuwaambia hana fedha ndipo
walipoanza kumcharanga mapanga.
Mtoto mkubwa wa Dk. Mvungi aitwaye Dk.
Natujwa Mvungi ameeleza kuwa baada ya watu hao kumjeruhi baba yake na
kufanikiwa kuondoka, walimchukua na kumkimbiza katika Hospitali ya Tumbi
mkoani Pwani ambapo amepatiwa huduma ya kwanza kisha kumkimbiza katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo baadaye alipelekwa kwenye wodi
katika Taasisi ya Mifupa (MOI) kwa ajili ya matibabu.
Dk. Mvungi aliwahi kugombea urais katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2005 kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuz
No comments:
Post a Comment