15 November 2013

BREAKING NEWZZ...HALI YAWA TETE KWA MH.MBUNGE Professor Juma Kapuya! MAKUNDI MBALI MBALI YATAKA AJIUZURU UBUNGE

Kufuatia kashfa ya kubaka na kumtishia binti: TAMWA, TGNP, LRHC wamucharukia Professor Juma Kapuya!

Washangazwa na Serikali kutochukua hatua zozote mpaka sasa; Wamtaka ajiuzulu Ubunge mara moja!

Endelea kusoma zaidi => http://bit.ly/1cvzino 
Tamwa, TGNP, LHRC wawacharukia viongozi
Na Mwandishi wetu
15th November 2013

Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa,Valerie Msoka
Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa), kwa kushirikiana na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na Kituo cha Msaada wa Kisheria (LHRC), kimelaani viongozi wanaotumia madaraka yao, nafasi zao na nguvu zao kisiasa kuwadhalilisha watoto wa kike.

Mashirika hayo yanayotetea haki za wanawake na watoto, yamesema yamesikitishwa na habari zilizozoripotiwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuhusu wasichana wawili wanaotafuta haki yao dhidi ya kiongozi wa kiserikali anayetuhumiwa kuwadhalilisha.

"Mashirika hayo yanafahamu kuwa vitisho vilivyotolewa na kiongozi huyo vimewasababishia wasichana hao kuogopa kuishi nyumbani kwao kwa kuhofia maisha yao," ilisema sehamu ya taarifa ya pamoja ya mashirika hayo.

Iliongeza: “Tunashangazwa kuona hakuna hatua zozote zilizochukuliwa na mamlaka husika wakati wasichana hao wakitafuta msaada," alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa, Valerie Msoka, katika taarifa hiyo.

Masharika hayo yametoa wito kwa mamlaka husika kuchukua hatua za haraka kuwalinda wasichana hao dhidi ya mtuhumiwa.
Aidha, ili kujenga imani na utawala bora, mashirika hayo yamemtaka mbunge huyo kujiuzulu mara moja.

Alisema Tamwa, TGNP na LHRC, yanawataka Watanzania kuungana na kupinga viongozi wanaotumia madaraka yao vibaya. Watanzania wapige vita vitendo visivyo vya haki kwa kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria.

CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname