Wachezaji wa Tanzania wakishangilia mabao 10-0.
Shelder Boniface akichezewa rafu na beki wa Msumbiji, Esperanca Malaita
Theresa amepiga krosi.
Bao la kwanza lilifungwa dakika ya sita na Neema Paul aliyeunganisha
pasi ya Theresa Yona, kutoka wingi ya kushoto, wakati mfungaji bora wa
michuano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars iliyofanyika mwaka huu
Nigeria, Shelder Boniface alifunga la pili dakika ya 24 baada ya
kupangua ngome na kumpiga chenga hadi kipa.
Deonesia Daniel akafunga bao la tatu kwa shuti kali la mpira wa adhabu
lililotinga moja kwa moja nyavuni dakika ya 32 na dakika ya 41, Amina
Ali akafunga la nne kwa shuti kali kutoka nje ya eneo la mita 18.
Tanzanites walipata bao la nane dakika ya 86 kupitia kwa Deonesia Daniel
aliyefunga kwa mkwaju wa penalti, baada ya Shelder Boniface kuangushwa
kwenye eneo la hatari.
Dakika ya 89 Tanzania ilipata bao tisa kupitia kwa Amina Ali tena,
ambaye alikuwa nyota wa mchezo huo. Stumai Abdallah akaifungia Tanzania
bao la 10 dakika ya 90.
Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Celina Julius, Stumai Abdallah, Maimuna
Said/Amina Hebron dk60, Fatuma Issa, Anastazia Anthony, Deonisia Daniel,
Vumilia Maarifa, Amina Ali, Neema Paul, Shlder Boniface na Theresa
Yona.
Msumbiji; Paulina Jambo/Catarina Francue dk50, Esperanca Malaita/Delice
Assane dk52, Felismisa Moiane, Emma Paulino, Gilda Macamo, Deolinda
Gove, Jessica Zunguene, Cidalia Cuta, Nelia Magate, LonicaTsanwane na
Onesema David.
Habari na picha kwa hisani ya Bin Zubeiry
No comments:
Post a Comment