Kama umeshushwa thamani unakuwa
kwenye hatari ya kuachwa. Hata kama mwenzako alikuwa ameshafikiria suala
la kuingia kwenye ndoa na wewe lakini kwa sababu ameshakushusha thamani
ndoa inaweza kuyeyuka.
Ukiwa kwenye ndoa ni hatari zaidi
maana mwenzako hukuchukulia wa kawaida – mazoea huzidi na hapo ndipo
uhitaji wa kuwa na mwingine wa pembeni unapoanzia. Haoni cha muhimu tena
kwako, ndiyo maana wazo hilo huvamia ubongo wake kwa kasi sana.
Itafikia hatua, kama upo ndani ya
ndoa, mwenzako atagoma kuongozana na wewe na kama ikitokea hivyo
mkikutana na rafiki zake njiani hatakutambulisha. Hisia kwamba
hamuendani humwingia.
UNAFANYAJE SASA?
Kubwa unalotakiwa kufahamu rafiki
yangu mpendwa, suala la kupanda au kushuka thamani lipo mikononi mwako.
Yapo mambo ambayo ukiyazingatia, mwenzako hawezi kukuchoka na kufikia
hatua ya kukushusha thamani.
Tayari tumeshaona athari zake lakini
hapa sasa nataka kukupa mbinu ambazo ukiwa nazo makini basi itakuwa
rahisi kwako kubaki namba moja na mtu muhimu zaidi (ndiyo inavyotakiwa
kuwa) kwa mpenzi wako maana ni haki yako.
ANZIA MWANZO
Ni rahisi zaidi kulinda thamani yako
kuanzia mwanzo wa uhusiano wenu. Ikiwa tayari mmeshakomaa halafu tatizo
hilo likajitokeza, hutumika nguvu nyingi zaidi kulirekebisha kuliko
kujizatiti kuanzia mwanzo wa uhusiano. Ni mambo gani hayo? Twende hapo
chini.
CHUNGA KAULI ZAKO
Naomba ieleweke wazi kuwa mada hii ni
maalum zaidi kwa wanawake. Kitu muhimu cha kwanza kabisa kwa mwanamke
ambaye anataka kuilinda thamani yake kwa mpenziwe ni kupima sana kauli
zake.
Acha kuropoka hovyo, pima maneno yako
na ikiwezekana kama unadhani kuna jambo huna uhakika nalo usizungumze
kabisa. Katika eneo hili, uwe makini zaidi mnapokuwa na watu wengine.
Kama mwanamke usiwe mchangiaji hoja sana.
Utulivu wako unaweza kuwa silaha kubwa ya kukufanya ubaki na thamani yako kama mwanamke anayejitambua.
USIRUHUSU MAPENZI
Msichana mwenye kujitambua na
kufahamu thamani yake sawasawa hawezi kuruhusu mwili wake ujulikane na
mwanaume harakaharaka. Onesha unajitambua na usikubali kirahisi kuuacha
mwili wako uchezewe.
Mpe hoja; kwanza mapema, hajakuoa
wala kukuchumbia, haraka ya nini? Wakati unawaza kuhusu kutoa penzi
lako, lazima ufikirie kuhusu athari zinazoweza kukupata kwa kukurupukia
mapenzi. Mwanaume ambaye bado hamjachunguzana na huna uhakika naye wa
kutengeneza maisha, kichwani mwake hakuweki kwa asilimia kubwa.
Ukumbuke kwamba, ukipata matatizo
yoyote – binafsi au yanayosababishwa na uhusiano wenu, anakuwa hana
uwajibikaji wa asilimia kubwa kwa tatizo hilo. Utabaki wewe na matatizo
yako!
mpyaaaaaaaaaaaa
ReplyDelete