Wakati Rais Jakaya Kikwete akituma salamu za rambirambi kwa Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kutokana na
kifo cha Balozi Isack Sepetu, mke wa marehemu amelaumu baadhi ya
viongozi wa Serikali, akidai walimtelekeza mumewe kwa kushindwa
kushiriki kumuuguza badala yake kuachia familia pekee.
Mariam, ambaye ni mke wa pili wa Balozi Sepetu aliyefunga naye
ndoa ya kimila mwaka 1982, alisema mumewe enzi za uhai wake aliwahi
kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi, ikiwamo ya Ubalozi Urusi na
kwamba, kwa kutambua mchango wake, Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed
Shein aliagiza agharimiwe matibabu lakini hakuna hatua
zilizochukuliwa.
zilizochukuliwa.
Akizungumza jana nyumbani kwake, Sinza Dar es Salaam, Mariam
alisema alijaribu kuwasiliana na Wizara ya Afya Zanzibar, lakini
hakupata ushirikiano aliopata, aliamua kumsafirisha mumewe huyo kutoka
Zanzibar hadi Dar es Salaam Oktoba 24, mwaka huu na kumpeleka Hospitali
ya TMJ Mikocheni.
“Nishukuru watoto wake wote waliungana na kushiriki kikamilifu kumuuguza
baba yao, wakishirikiana na ndugu na jamaa zetu wachache. Kwa kweli
jambo hili limenihuzunisha sana nafikiri
hakupata huduma ya kutosha,” alisema
No comments:
Post a Comment