30 October 2013
HIZI NDO FUJO ZILIZO FANYWA NA MASHABIKI WA MBEYA CITY KATIKA MCHEZO DHIDI YA PRISON
Taarifa kutoka 87.8 Mbeya zinaamplfy kwamba mashabiki wa Mbeya City wamelishambulia gari la wachezaji wa Prisons na kumuumiza mchezaji mmoja ambapo pia walivunja vioo vya gari aina Toyota Coaster na magari mengine yaliyokuwa kwenye msafara wa timu hiyo ikitoka uwanjani baada ya kufungwa na Mbeya City kwa mabao 2-0.
mbeyayetu.blogspot.com wameripoti kwamba Mashabiki hao walilishambulia magari hayo na kuyavunja vioo na baada ya hapo wakakimbilia kusikojulikana.
Mmoja wa maofisa wa Prisons alisema ana uhakika kuwa waliofanya hivyo ni mashabiki wa Mbeya City kwa kuwa walikuwa wamevaa jezi za rangi ya zambarau ambayo huvaliwa na timu hiyo.
Hapa chini ni baadhi ya fans Mbeya City wakiwa wamebeba jenela la timu ya Prisons, chini ya hii picha ni baadhi ya picha wakishangilia magoli uwanjani
credit-mbeyayetublog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment