12 May 2013

BREAKING NEWS: MANCINI ATIMULIWA KAZI MANCHESTER CITY, PELLEGRIN AKABIDHIWA NAFASI YAKE


Mancini

Roberto Mancini sasa si kocha mkuu tena wa Manchester City, imeelezwa.


Nafasi ya Muitaliano huyo itachukuliwa na kocha wa Malaga, Manuel Pellegrini.


Bado haijajulikana rasmi ataondoka leo usiku, kesho au keshokutwa lakini inaonekana hakuna uhakika kama atakuwepo kwenye benchi kesho wakati City watakapokuwa wakiivaa Reading.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Man City zinaeleza, uamuzi
wa kumtimua Mancini ulichukuliwa katika kikao cha pamoja kilichowajumuisha mabosi wawili Ferran Soriano, Txiki Begiristain na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Khaldoon Al Mubarak ikiwa ni siku moja tu baada ya City kuchapwa bao 1-0 katika mechi ya fainali ya Kombe la FA.


The Sun la Uingereza lilifanya juhudi za kumnasa Mancini ili azungumzie suala hilo lakini haikuwezekana lakini kumekuwa na taarifa amebanwa kwa kuwa anashughulikia suala la malipo ya fedha zake baada ya mkataba wake kusitishwa.

Ingawa yeye alisema jana amebakiza miaka minne na City, lakini taarifa zinaeleza ana miaka mitatu iliyosalia na alisaini baada ya kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu England.

Jana, Mancini aliushambulia uongozi wa City kwa madai haukuonyesha juhudi za kukanusha kwamba ulikutana na wakala wa Pellegrin na aliyehusishwa kufanya naye mazungumzo ni Txiki.

Taarifa za Txiki kukutana na wakala wa Pellegrini zilianza kuchukua nafasi tokea wiki iliyopita na uongozi wa City ulionekana kuwa kimya kabisa kuhusiana na suala hilo.

Pamoja na kuipa City ubingwa wa Ligi Kuu England, Mancini aliibebesha Kombe la FA msimu huu.

Kwa kifupi, msimu huu pamoja na kushika nafasi ya pili, wamevulikuwa makombe yote waliyokuwa nayo msimu huu na uliopita.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname