JESHI
la Polisi mkoani Singida linamtafuta kijana mmoja mkazi wa Kibaoni
katika manispaa hiyo kwa tuhuma za kumlawiti mwenzake na kumharibu
vibaya sehemu za haja kubwa baada ya kumnunulia pombe kali aina ya
viroba jogoo tisa.
Kamanda
wa polisi mkoani hapa, Geofrey Kamwela, alisema kuwa tukio hilo
lilitokea juzi saa 3:00 usiku eneo la soko la Kibaoni, kata ya Kindai,
na kumtaja mtuhumiwa huyo kwa jina moja la Athuman.
Alisema
kuwa baada ya kila mmoja kumaliza kunywa viroba vyake, kijana
aliyelawitiwa (jina tunalihifadhi) alimweleza mtuhumiwa kuwa amelewa
kupindukia na hivyo kila mmoja arejee nyumbani kwao.
“Walipofika
eneo la soko la Kindai, muathirika alimwambia mtuhumiwa amwache hapo
ili apumzike kwa vile pombe ilikuwa imemzidi sana lakini ghafla
alianguka chini na kisha na kupoteza fahamu,” alisema.
Baada ya muathirika kupoteza fahamu, mtuhumiwa alitumia fursa hiyo na kuanza kumwingilia kimwili kinyume cha maumbile.
Alisema
kuwa wasamaria wema walimshuhudia mtuhumiwa akiendelea kufanya unyama
huo dhidi ya rafiki yake lakini walipojaribu kumkamata, aliwaponyoka na
kukimbilia kusikojulikana.
“Raia
wema hao walimbeba muathirika na kumpeleka nyumbani kwake na baadaye
aliweza kupata fahamu ndipo alianza kusikia maumivu makali sehemu yake
ya haja kubwa,” alisema.
Alisema muathirika alipelekwa hospitali ya mkoa wa Singida ambako alibainika kuharibiwa vibaya sehemu zake za haja kubwa.
No comments:
Post a Comment