Pamoja na kwamba kaka yake, Diamond kuwa
msanii mkubwa na mwenye mafanikio, Queen Darleen hafikirii kufanya
collabo naye hivi karibuni.
Akizungumza na Bongo5, msanii huyo wa
siku nyingi amesema hana haraka kwakuwa Diamond anamuona kila siku na
bado anataka akue zaidi ya hapo.
“Nafikiri mimi namchukulia ni mdogo
wangu na ninaamini kwamba yupo na ninampa nafasi aendelee kufanya kazi
nzuri zaidi. Kwasababu nikifanya naye sasa hivi ntakuwa nimepoteza maana
nzima ya udugu,” alisema Queen.
“Kila siku akija namwambia bado, bado
kufanya nyimbo na mimi. Najua kwamba yupo juu zaidi yangu lakini still
kwangu yupo chini sababu mimi ni dada yake na ananiheshimu na mimi
namheshimu.”
Amesema kila kitu anachofanya Diamond humshirikisha dada yake huyo na yeye amekuwa mshauri wake mzuri.
“Hawezi kutoa nyimbo redioni bila kunisikilizisha mimi, si yeye, si Dully Sykes, si Ali Kiba, wote wako hivyo.”

No comments:
Post a Comment