10 September 2013

Dada zangu hivi ni Vitu ambavyo vinaweza kumfanya mwanaume asikuone una mvuto pamoja na uzuri wako

 
Mavazi yasioendana na tukio: Unakuta mwanaume amemualika mrembo kwenda ku dine mahali fulani anakuja na mavazi kama vile anakwenda kununua koni kwa Bakhresa Kariakoo.
Ni vyema mwanamke kama amealikwa mtoko ajue anapelekwa wapi ili asije akakchekesha bure.
Ngoja niwape siri moja, kwa taarifa yeni ni kwamba, hata mwanamke awe ni mrembo kiasi gani, lakini kama kavaa kituko ana m put off mwanaume kabisa na hamu yote inamuisha

Nywele zisizovutia: una wakti unaweza kuwa na miadi ya mtoko na mdada, ukijua kwamba atakuja ametokelezea, lakini akija unaweza ukatamani kumkimbia maana huo mtindo wake wa nywele wala hauna mvuto. anaweza kuwa amevaa vizuri lakini nywele zake mh! utadhani ndio ametoka kulala

Usafi kunako eneo husika. 
Kusema ukweli lile eneo husika likiachwa na kichaka linatisha, hata kama mwanamke awe mzuri kiasi gani, lakini kama eneo husika halijalimwa vizuri na kuwekwa nadhivu, mwanaume hawezi kuuona uzuri wa mwanamke huyo, hamu yote itamtoka.




Kucha mbaya zisizo na mvuto na visigino kama msasa:
Duh, unakutana kucha ni eneo lingine ambalo linaweza kumfanya mwanaume akamuona mwanamke kuwa asiyevutia kama hazitafanyiwa matengenezo na kunakshiwa kwa rangi au kupigwa polish mara kwa mara.

Ni vyema mwanamke kabla ya mtoko kukagua kicha zake zisije kuwa na sharp edges ambazo zinaweza kumkwaruza mwanaume wakati wa ku hug, pia kule kwenye kisigino nako kunakuwaga na msasa, mwanamke anashauriwa kuhakikisha anaondoa msasa wa kisigino ili kuleta mvuto, sio unamkanyaka mwanaume kwa mahati mbaya anahisi kapitiwa na Grander 



Ghubu na kukasirika hovyo:
Kuna wanawake wana drama jamani usiombe kukutana na mwanamke asiyetabirika, muda huu anacheka muda kidogo kanuna, bila sababu au unakuta tu kalianzisha kisa tu mwanaume amesafisha kiwi cha macho kwa kukata shingo kuangalia makalio ya wanawake wengine.
Au ndio mko kitandani kwa maandalizi ya kuelekea kunako utukufu mara akakumbuka kitu mlichotofautiana mwaka juzi akalianzisha. 

Source:Jamii forum

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname