STAA wa filamu za Kibongo, Wastara Juma,
yeye ameamua kula Sikukuu ya Idd El Fitr kwa staili ya tofauti na watu
wengine ambapo alikula kaburini kwa mumewe, marehemu Juma Kilowoko
‘Sajuki’.
Ishu hiyo ilijiri Ijumaa iliyopita siku
ya sikukuu hiyo ambapo Wastara alitundika picha zake zikiwa zinamuonesha
akiwa ameshika tama na nyingine akiwa analifanyia usafi kaburi la
marehemu Sajuki lililopo katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar.
Wastara alikiri kuwa aliitendea haki
Sikukuu ya Idd kwani alipata nafasi ya kuzuru kaburi la mumewe na
kujisikia faraja japo kimwili hayupo naye lakini kiroho wako pamoja.
“Sikukuu yangu nimeitendea haki sana kwa
kwenda kuzuru kaburi la mume wangu, alhamdullilah nimefarijika sana,
kimwili siko naye ila atabaki kuwa fikrani mwangu milele,” aliandika
Wastara.
Mashabiki wake na wadau mbalimbali
walimpa pole huku wengine wakimpongeza kwa hatua hiyo kwani wasanii
wengine waliotumia sikukuu hiyo kujiremba, kwenda klabu na kujirusha.
Sajuki alifariki dunia Januari 2, mwaka huu na kuacha mtoto mmoja wa
kike.
Source:Global Publisher

No comments:
Post a Comment