31 August 2013

KOMBATI ZA JESHI LA RWANDA ZIMEKUTWA CONGO BAADA YA M23 KUTELEKEZA NGOME YAO

Kufuatia kichapo kiakali walichokipata waasi wa M23 na kulazimika kurudi nyuma takribani km 10 sasa na kutelekeza ngome yao imebainika baadhi ya magwanda ya kijeshi yaliyokutwa ni ya jeshi la rwanda. 
Kwa mujibu wa taarifa ya aljazeera rwanda imeendelea kukanusha kwamba hawahusiki na na mapigano hayo licha ya sare zao za kijeshi kuokotwa eneo hilo.ilikuwa ngome imara iliyokuwa na maandaki ya kutosha na strategical sana lakin tangu jwtz wamue kuwasambaratisha wameyatelekeza.baadhi ya wanajeshi wa drc waliohojiwa mawetupia shutuma moja kwa moja rwanda na kusema kwamba congo ni ya wakongo wala si ya warandwa wala ya wa M23.
Source; aljazeera

my take ni kwamba sasa kagame kaumbua kweupe ama kweli kucheza kwingi mwisho kukaa kuchi na kuchamba kwingi mwisho kukomba mavi na sikuzote chizi hajijui angekuwa anajijua asingeokota makopo jalalani

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname