31 August 2013
HIVI UMALAYA NI TABIA AMA KUTORIDHIKA NA MPENZI MMOJA?
Habari wana jamvi, ni matumaini yangu hatujambo sote. Jamani me nina tatizo moja naomba mchango wenu. Niliolewa na mume wangu halali kabisa wa ndoa. Mwanzoni tulipendana sana, lakn gafla mwenzangu akachange akawa mkali kwangu bila sababu, anachelewa kurudi cku nyngne harud kabisa. Sikuwah kumfokea wala kumuulza ulikuwa wapi, nilimpokea tena kwa mahaba yote niliyofundshwa na bibi yangu, nampa chakula anakataa, nampeleka bafuni namuogesha na ninagundua kabisa mume wangu ametoka kwa mwanamke mwingne, lakin nampa haki zake zote za msing.
Ilifkia kpnd natukanwa na wanawake zake kny cm, lakn yeye haoneshi hata kushtuka. Cjawah kumshatki hata kwa mshenga, nilikuwa namvumilia najua ndo mume nimepewa na mungu. Kilichokuja kutokea ni kwamba alihama nyumbani akaniacha na wanangu wadogo ni mapacha wenye umri wa mwaka1, nimewalea mwenyewe kwa shida hvyo hvyo na vibiashara vyangu mpaka leo, ikafikia cku wakaja ndugu zake kunifukuza kwenye nyumba ile nikarud kwetu na wanangu. Huko nikaona nimfuate mshenga nimweleze, mshenga akamuita, alipomuita alikuja na ndug zake hao wenye maneno yani washari balaa, basi ktk kuongea ikanekana wanandugu walipanga tangu huko kwao kwamb waje kuivunja ndoa yangu, mume wangu bila ya huruma akanipa talaka mbele ya ndug zake na wanangu wakilia kwa uchungu kama walijua kilichokuwa kinaendelea.
Nikaanza maisha ya upweke na wanangu. Cha ajabu baba yao huwa anakuja analia eti nimsamehe tulee watoto we2. Anasema et yey hapendi kuwa malaya ila inatokea tu . Nisaidien wajameni, me cmpendi hata kidogo yan amenitoka kabisa kwa jnc alivyonitenda na hawa malaika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment