13 June 2013

BABA YAKE LANGA,MZEE KILEO AMESEMA MWANAE LANGA AMEFARIKI LEO,TARATIBU ZA MAZISHI ZITATOLEWA BAADA YA VIKAO VYA FAMILIA

Baba wa marehemu Mzee Kileo amesema kuwa mtoto wake Langa kwenye picha amefariki dunia leo majira ya saa 10 katika hospitali ya Taifa Muhimbili.Taarifa kamili na mipango ya mazishi zitatolewa pale vikao vya familia vitakapofanywa.Pia baba yake alisema msiba huu umetokea wakati mama yake Langa hayupo Tanzania,alisema kwa sasa mama yake Langa yupo Marekani lakini baada ya kupewa taarifa hizo tayari ameshakata tiketi ya kurudi Tanzania na ataanza safari kesho.Msiba uko nyumbani kwao maeneo ya Mikocheni
#RIP Aarif!

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname