Kamanda diwani akiwaonyesha moja ya jambazi lililokuwa limeshika silaha
Hii ndiyo Gari iliyotumiwa na majambazi hayo
Siraha walizokuwa wanatumia majambazi hayo
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amewaambia Wandishi wa Habari
Ofisini kwake kuwa Tukio hilo limetokea leo majira ya saa Sita Mchana katika
kijiji cha Garijembe Wilaya ya Mbeya katika Barabara ya Mbeya Tukuyu.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amewaambia Wandishi wa Habari
Ofisini kwake kuwa Tukio hilo limetokea leo majira ya saa Sita Mchana katika
kijiji cha Garijembe Wilaya ya Mbeya katika Barabara ya Mbeya Tukuyu.
Alisema baada ya
Jeshi la Polisi kupata taarifa za Kinterejensia waliweka mitego mbali
mbali na kufanikiwa kuwanasa watu hao wakiwa kwenye gari lenye namba za
usajili T 911 BUG aina ya Toyota Spacio.....
Baada ya kusimamishwa ghafla walianza kurusha risasi ovyo ambapo
Askari walijibu mapigo na kufanikiwa kuwajeruhi wote watano ambapo
waliwafikisha katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya Matibabu
lakini Daktari alithibitisha kuwa tayari walikuwa wamekufa.
Aliongeza
kuwa baada ya kufanyiwa upekuzi walikutwa na Silaha mbili ambazo ni
bunduki aina ya SMG 848628 ambapo kwenye magazine zilibaki risasi 16 na
bunduki nyingine aina ya Mark III yenye namba 94695J ikiwa na risasi
mbili pamoja na Koa za Shaba.
Kamanda
Diwani ameongeza kuwa taarifa za Kinterejensia zilieleza kuwa majambazi
hayo yalijipanga kufanya uhalifu katika maeneo ya Ushirika, Tukuyu
Mjini Wilayani Rungwe pamoja na Eneo la Uyole Jijini Mbeya.
Aidha
alisema majina yao wala makazi yao hayakuweza kujulikana mara moja
ambapo miili yao imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na kutoa wito
kwa wananchi kufika Hospitalini hapo kwa ajili ya kuwatambua ndugu zao
ili wakabidhiwe kwa taratibu za mazishi.
Pia anatoa wito kwa wananchi wenye taarifa zinazohusu uhalifu kuzitoa katika mamlaka zinazohusika kwa wakati ili zifanyiwe kazi.
Mbeya yetu
Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment