07 April 2013

Chid Benzi na Producer Lucci Wahamishia Ugomvi wao Twitter ili kila mtu aone

Rapper Chidi Benz na producer Lucci wameingia kwenye mgogoro baada ya kutofautiana katika makubaliano ya wimbo walioufanya pamoja. Chidi anamlaumu Lucci kwa kubadilisha msimamo wake ambapo alidai kumfanyia wimbo huo bure.

Chidi Benz na Lucci wametumia Twitter kulizungumzia
suala hilo kama ifuatavyo:

Chidi Benz: Unachofanya c sawa.usipindishe maneno na usifoc makubaliano.siku tunarekod hukusema khs mkwanja,ulisema tufanyeni kazi.u mi n kk

Lucci: Ofisi na simu zipo, KWELI kuna haja ya kuhusisha watu zaidi ya 7,000? Kwani walikwepo tukifanya kazi? B professional and call me

Chidi Benz: Unahisi hio ni point koz unajaribu kutafuta points.tym tunarekod ulitweet na ukifurahia.mnakimbiliaga huku mwisho.mimi m real. Professional ni wewe kuchange deal,hatuna lazima ya hio kazi but haukua mpango uliopangwa,tumetumia energy.Tamaa imekubadilisha.

Lucci: Kwani mimi sijatumia energy?!? Mara ngapi nimekuambia uje ofisini tuandikishane makubaliano? Hata vya BURE hua na maandishi.

Chidi Benz: Hakukuwa na bure,hatukutaka koz hatukuingia na force kwenu wala hatukuvunja mlango.thou ulituelekeza studio ilipo.Nakuona…

Lucci: Ulitumiwa email ya mkataba na ofisi yangu @TransforMaX_R HUKUJIBU wala hukusema terms unazotaka. JE, nifanye lipi la ZIADA?

Chidi Benz: Unafanya kazi ndio unapewa mkataba au unapewa mkataba kisha unafanya kazi? KK ananambia khs mkataba na mi sina mail. Studio ipo kwenu ndani chumbani I thnk pale,unahisi mtu anaweza toka Ilala na hajui terms zako?hajui anakuja kufanya nini?

Lucci: Cha msingi ni mkataba, na hicho ndiyo kilio changu. Chumbani, Jikoni, kote kazini.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname