Tatizo
la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa wanandoa na
wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu ndoa 4 kati ya 10
zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliana na tatizo hili. Aidha wanaume
6 kati ya 10 wanatajwa kulalamikia upungufu wa nguvu za kiume na kuacha idadi
ya wanawake wanaokabiliwa na tatizo hilo
kwa mujibu wa uchunguzi kubaki na asilimia 13.
Pamoja
na matatizo mengine kutajwa kuchangia upungufu wa nguvu za kiume na kushuka kwa
msisimko wa tendo miongoni mwa wanandoa, uchunguzi umeonesha kuwa utumiaji
holela wa vyakula hasa vyenye mafuta ni moja kati ya sababu zinazochangia kwa
kasi tatizo hili.
Kwa
kuzingatia hilo,
watafiti wa masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini aina kumi ya vyakula
ambavyo vina uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya kufanya tendo la ndoa. Vyakula hivyo ni hivi vifuatavyo:
PILIPILI
Pilipili zilizocheshwa zimetajwa kuwa na uwezo wa
kusaidia msukumo wa usambazaji damu mwilini, ambao kwa kiasi kikubwa ndiyo
unaoweza kumfanya mtu akawa na hisia kali za kimapenzi. Kwa msingi huo, ni vema
kwa wale wanaokabiliwa tatizo la uwezo wa kufanya mapenzi wakatumia pilipili si
kwa wingi bali kwa kiwango stahili, ili waamshe hisia zao.
PARACHICHI
Aina
nyingine ya chakula ambacho husaidia kuongeza uwezo wa mtu kufanya tendo la
ndoa ni Parachichi. Tunda hili linauwezo mkubwa wa kuzalisha vitamini E ambayo
husaidia katika uzalishaji wa homoni. Inatajwa kuwa watu wanaotumia tunda hili
kwa wingi huwana msisimko mkali wa kimapenzi na kwa upande wa wanawake husaidia
kuongeza majimaji yenye utelezi sehemu za siri na hivyo kuzuia uwezekano wa
kuchubuka wakati wa kujamiiana.
NDIZI
Wakati
unafikiria uwezo wa kufanya vema tendo la ndoa unatakiwa kuwaza juu ya uimara
wa misuli ya mwili ambayo inatajwa kuwa ni sehemu kuu na yenye muhimu katika
kujamiiana. Kwa msingi huo ulaji wa ndizi mbivu unatajwa kusaidia kujenga
misuli mwilini na kumfanya mtu aweze kuwa hodari katika tendo la ndoa.
CHOKOLETI
Ulaji wa
Chokoleti huongeza uchangamfu mwilini na, hivyo kumuwezesha mtu anayeshiriki
tendo la ndoa kuwa na mguso sahihi kwenye fikra zake, jambo litakalomuwezesha
kupokea hisia za mapenzi kwa urahisi zaidi ya mtu ambaye anakwenda kwenye
uwanja wa sita kwa sita akiwa mchovu wa mawazo.
CHAZA NA
PWEZA
Aina
hizi za samaki zinazovuliwa baharini huwa na madini ya zink na chumvi ambayo
yanatajwa kusaidia uzalisha wa vichocheo vinavyohamasisha msisimko wa mwili
wakati wa tendo la ndoa.
POMEGRANATE
Ni aina fulani
ya matunda mekundu yanayofananana na apple.
Haya yatajwa kusaidia kuamsha mishipa ya fahamu na kuweka mawasiliano sahihi ya
mwili na hivyo kumuongezea mtu uwezo kwa kufanya tendo la ndoa kwa hamasa
kubwa.
MVINYO
MWEKUNDU
Mvivyo
mwenyekundu unatajwa kuwa na uwezo wa kuuchangamsha mwili na kuongeza msukumo
wa damu, kiasi cha kumuondolea mtu uchovu kabla na baada ya tendo la ndoa,
hivyo ni muhimu kunywewa hasa na wale ambao wanasumbuliwa na tatizo la
kushindwa kurudia tendo.
MBEGU ZA
MATUNDA
Mchangayiko
wa mbegu mbalimbali za matunda, mfano tikiti, maboga husaidia kuondoa ACID
mwilini na kumfanya mtu ajione ni mwenye afya njema.
VANILLA
Vanila
husaidia kuamasha hamasa mwili.Mwisho wa aina hizi za vyakula ni TIKITI MAJI
ambalo linatajwa kuwa na virutubisho vingi vyenye uwezo wa kuusaidia mwili kuwa
na nguvu za kutosha kufanya tendo la ndoa.