Ikiwa
ni miezi mitatu tu imepita toka nchi nyingine ambayo ni maarufu Afrika
(Kenya) kukumbwa na headlines za kutosha kuhusu raia wake wanaoshiriki
mapenzi ya jinsia moja kupeana tuzo hadharani na kufanya sherehe, leo
tena headlines zimehamia Nigeria.
Ndani
ya miaka mitano iliyopita huko Nigeria kulikua na Kanisa ambalo lina
waumini wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja tu liitwalo House of Rainbow
lakini Kanisa hilo lilipotea baada ya kushambuliwa na wakazi wa Lagos
ambao hawapendezwi na ishu za ushoga na usagaji.
Tarehe
3 March 2013 Mtandao maarufu wa Nigeria wa TFJ umeripoti kwamba kanisa
hilo limerejea tena kwa kishindo na kuendelea na huduma zake.
Ni
kanisa ambalo mwanzilishi wake ni mchungaji Mnigeria ambae ni shoga
Rowland Jide Macaulay na imefahamika sasa hivi kwamba kanisa hilo lipo
Ghana na Malawi, France, Netherlands, Cote d’Ivoire na Sierra-Leone.