Kwa mujibu wa website ya MalawiVoice, Serikali ya Malawi imemfukuza
balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mh. Patrick Tsere, na kumpa masaa 48
aondoke nchini humo. Ripoti zilizotoka ikulu ya
Malawi zinasema Mr.
Tsere ametajwa kuwa ni person-non-grata, ambayo katika ulimwengu wa
diplomasia, inamaanisha ni mgeni asiyekaribishwa, na serikali ya nchi
hiyo imekata mawasiliano ya kidiplomasia na mwanadiplomasia huyo.
Hatua hii imefuatia mahojiano aliyofanyiwa Mr. Tsere na gazeti la
Zodiak Malawi ambapo alitamka wazi kwamba nusu ya ziwa Nyasa baada ya
mpaka wa Msumbiji, inamilikiwa na Tanzania.
“Hili sio ziwa Malawi. Ni ziwa Nyasa. Linamilikiwa na mataifa yote
yanayolizunguka, Tanzania, Malawi na Msumbiji.” Alisema Mr. Tsere katika
mahojiano hayo
Ripoti hiyo inasema Mr. Tsere amepewa masaa 48 aondoke Malawi. Malawi
hivi karibuni imekua ikiishutumu Tanzania kupeleka wanajeshi kufanya
doria kwenye upande wa ziwa ambao Tanzania inadai ni wakwake. Pia ripoti
hiyo imelalamika kwamba askari hao wa Tanzania wamekua wakiwanyanyasa
na kuwakamata wavuvi wa Malawi kwenye upande wa ziwa ambao Tanzania
inadai ni wakwake.
Tukio hilo limekumbusha wakati rais wa Malawi aliyepita, hayati Bingu
wa Mutharika alipomfukuza balozi wa Uingereza nchini Malawi.
source- www.
source- www.