Kama unatumia simu ya Android na unapenda kutunza chaji, huna budi
kufuta app moja muhimu, imebainika. Tatizo ni kwamba app hiyo ni
Facebook – ambayo watumiaji wengi wanaichukulia kama moja ya app muhimu.
Ripoti zinadai kuwa ukitoa app hiyo, uhai wa betri ya simu huongezeka
kwa asilimia 20 pamoja na kuongezeka speed. Inashauriwa kutumia Facebook
kwa kutumia browser ya Chrome inayotoa notifications kama app tu.
No comments:
Post a Comment