Sumu ni kitu chochote kile ambacho katika mwili huhatarisha utendaji
kazi wa mifumo au viungo vya mwili na huweza kupelekea kifo.
Kwa kutegemeana na namna ambavyo sumu huuathiri mwili, tunapata makundi
mawili ya sumu; Kundi la kwanza ni aina za sumu ambazo husababisha
madhara yasiyorekebishika au tuite ulemavu wa maisha (Irreversible
effects), na kundi la pili ni aina za sumu zinazosababisha madhara
yanayoweza kurekebishika (Reversible effects).
Miongoni mwa madhara yasiyorekebishika yanayoweza kusababishwa na kundi
la kwanza la sumu ni pamoja na, makovu katika ngozi, upofu, matatizo ya
akili, matatizo ya damu, kulemaa au kupooza viungo na kuwa kiziwi.
Kundi la pili la sumu husababisha madhara yanayoweza kurekebishika au
kutatulika baada ya muda fulani, mfano uvimbe, kuwasha kwa ngozi, ngozi
kuwa kavu sana, kutokwa na majibu pamoja na sehemu za mwili kubadilika
rangi.
Mpenzi msomaji, kuna vyanzo viwili vya sumu mwilini; chanzo cha kwanza
ni kupitia vitu ambavyo vipo nje ya mwili, binadamu huvitumia na matokeo
yake humuathiri. Vitu hivi MTU huvitumia pengine kwa kujua au kutokujua
kuwa kwake ni sumu, mfano matumizi ya kemikali aina ya zebaki (
mercury) katika shughuli za migodini, uangalifu au umakini mkubwa
wahitajika pindi utumiapo kemikali hii kwani huweza kukupa madhara
katika mapafu na moyo. Sumu nyingine hujitokeza kwa kukosa au
kutozingatia maelekezo tunayopewa juu ya utumiaji salama Wa Dawa za
kutibu magonjwa, mtu anazidisha dozi, au ni mama mjamzito lakini
anatumia Dawa ambayo siyo salama kwa kiumbe kilichopo tumboni, matokeo
yake ni kuhatarisha maisha ya mjamzito, mtoto tumboni au kuja kujifungua
mtoto mwenye ulemavu usio rekebishika.
Chanzo cha pili cha sumu ni miili yetu wenyewe, ni katika hali ya
kawaida mwili unazalisha sumu mbalimbali kupitia mifumo yake ya Kazi,
mfano katika uvunjwaji na usambazaji Wa chakula mwilini, mifumo ya hewa,
utengenezaji wa damu, katika Kazi zote hizi na nyingine ambazo mwili
hufanya, kuna baadhi ya sumu huzalishwa pamoja na kemikali (free
radicals) nyingi ambazo hazitakiwi ziendelee kukaa mwilini, kwani
huathiri utendaji Kazi wa kawaida wa mwili.
Uondoaji wa sumu mwilini hutegemeana na aina ya sumu yenyewe. Njia ya
kwanza ni matumizi ya Dawa za kuivunja nguvu ile sumu husika ambapo
kitaalamu hujulikana kwa jina la antidote, hapa ni baada ya uchunguzi
kufanyika na kugundua aina ya sumu iliyokuathiri na kisha utapewa dawa
kulingana na majibu ya uchunguzi wa kitaalamu.
Njia ya pili inayoweza kutusaidia kuondoa sumu na hasa zile
zinazozalishwa mwilini ni matumizi ya vyakula bora, hivi ni vyakula
ambavyo kwa asili yake huwa na virutubisho ambavyo huvunja vunja na
kuondoa sumu mwilini, vyakula hivi kitaalamu huwa na vitu vinavyoitwa
antioxidants, ambavyo huulinda mwili dhidi ya kemikali hatarishi
zinazozalishwa mwilini. Virutubisho hivi ni pamoja na Vitamin A,
Vitamini C na Vitamini E. Vitamini hizi hupatikana katika mboga za
majani na matunda, mfano mchicha, spinachi, karoti, matembele,
machungwa, nanasi, maembe, machenza pamoja na mafuta ya mimea mfano
alizeti.
Ili miili yetu iweze kufanya kazi vizuri na tuendelee kuwa na afya
njema, inabidi tuepukane na sumu hizi, pale inapo tulazimu zitumike
(mfano zebaki, migodini), basi tuzidishe umakini katika kujilinda afya
zetu, na pia tubadilishe aina ya maisha au ulaji wa vyakula, matunda na
mboga za majani ni walinzi wakubwa sana wa afya zet
No comments:
Post a Comment