Julius Malema na wafuasi wake wakitoka bungeni'
Kumetokea
malumbano makali bungeni nchini Afrika Kusini ambapo wanasiasa wa
upinzani wamechelewesha hotuba ya rais Jacob Zuma aliyekuwa akilihutubia
taifa na kuzua maswali kuhusu utaratibu.
Baadhi ya wanasiasa wanasema rais huyo hakupaswa kuhutubia bunge kutokana na kashfa mbali mbali alizonazo
Ni
mvutano huo baada ya spika wa bunge la Afrika Kusini mama Baleka Mbete
na wafuasi wa upinzani wengi wao kutoka chama cha Ecoomic Freedom
Fighters EFF wakiongozwa na Juliasi Malema ambao walikuwa wanadai kutaka
utaratibu na kuvuruga hotuba ya Rais Jacob Zuma..
Hatimaye
uvumilivu ukamshsinda spika wa bunge Baleka Mbete na kumuru kiongozi wa
EFF Julias Malema kutolewa nje ya ukumbi wa bunge.
Baada ya fujo hizo Rais Jacob Zuma alijaribu kuendelea kuhutubia lakini wabunge wa upinzani walibaki wakarudia tena kumkatiza
Baada
fujo hizo baadae angalau kidogo pakawa na utulivu ambapo Rais Zuma
aliweza kumalizia hotuba yake na Katika hotuba hiyo Rais Zuma mbali na
mambo mengine alisema serikali yake imekuwa akibana matumizi lakini
anaona bado hatua zaidi zinahitajika.
"Tumekuwa
tukichukua hatua za kubana matumizi ya fedha za umma kwa hekima ikiwa
ni pamoja na kubana matumizi yasiyo ya lazima. Lakini bila kuathiri
wajibu muhimu wa serikali na kutoa huduma kwa raia. Mwaka 2013 waziri wa
fedha alitangaza hatua za kubana matumizi. Matumizi ya ziada na yale
yasiyo ya lazima yamepunguzwa lakini bado hatua zaidi zinapaswa
kuchukuliwa kubana upotevu wa fedha za umma."
Rais Zuma
anakabiliwa na kashfa kadhaa lakini kubwa la hivi karibuni ni hatua ya
kutumia fedha za umma kufanya ukarabati wa kasri lake la kifahari la
Nkandla.BBC
No comments:
Post a Comment