09 February 2016

Mwanamke, kumchuna mumeo ni sawa na kujiibia mwenyewe

 

Naongea hivi maana wanawake wengi wa leo tunashindwa kutofautisha mume na mtu mpita njia au kwa maneno mengine mtu usie na uhakika nae kwamba mtaishi wote kama mume na mke.

Unakuta mwanamke keshaolewa badala ya kumshauri mume wake wajenge future yao ya baadaye na watoto wao, eye ndo kwanza yuko busy anataka wigi la laki sita, anataka viatu vya laki 3, anataka Iphone, nguo za Woolworth, starehe kwa sana na kushughulikia vya tumbo tu anasahau wako kwa nyumba ya kupanga wala hana habari.

Simaanishi kwamba wanawake waume zenu wasiwapendezeshe but acheni kudemand vitu visivyo na tija badala ya kujenga future yenu. Mambo ya kucompete na mashost zako so nawe unataka uonekane umo unamgeuza mumeo buzi wakati ni mume wacha.

Mwanamke bana matumizi vizuri, weka mahesabu yako sawasawa, mshauri mumeo mfanye mambo ya maana achana na mawigi ya laki 6, kufanya showoff wakati hamna nyumba maana kesho watoto hawatalala kwenye hilo wigi la laki 6.

Umeshaolewa maana yake mko na huyo mumeo kujenga kesho yenu itayokuwa the best.
Wachaneni na vitu visivyo na maana pindi mkishaolewa, msaidie mumeo kujenga future yenu na sio kumchuna maana ni sawa na unajiibia mwenyewe
CREDIT - JF

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname