Baraza la Sanaa nchini(BASATA) limeufungia wimbo wa Ney wa mitego
unaoitwa 'shika adabu yako' kutokana na matumizi ya lugha chafu ndani ya
wimbo huo. Akiongea leo na kituo maarufu cha redio, katibu mkuu
mtendaji wa baraza hilo amesema ni wimbo ambao haufai na anashindwa
kumpima Ney ana akili za namna gani.
"Kitu ambacho hakifai kwenye jamii sio mpaka litolewe tamko kwamba wimbo umefungiwa, ni wimbo ambao haufai hata wanajamii wameona haufai, nadhani mtu mwenye akili timamu kiujumla anajua, najua kwenye media hauwezi kupigwa”
Wimbo huo mpya kutoka kwa Ney wa Mitego ulisika Live kwa mara ya kwanza kupitia kipindi cha XXL.
Katika wimbo huo uitwao 'Shika Adabu Yako', Ney amewaumbua kwa kuwataja majina wasanii na watu maarufu nchini akianika ubovu wa matendo yao na kuwataka wabadilike.
Pia katika wimbo amewaimba baraza la Sanaa la Taifa(BASATA) kwa kuwaita ni msumeno usiokata na kazi yao ni kufungia nyimbo ilhali hawajui shida wanayopata na kama wangekuwa watoto angewachumia fimbo.
Pia hakumuacha nyuma Magufuli na serikali yake kwa kusema amezoea wasanii ndio watu wanapenda umaarufu lakini safari hii ligi ya umaarufu ipo kwenye serikali kwa kila kiongozi kuwa na mwandishi kisha kushindana magazetini.
DOWNLOAD HUO WIMBO HAPA CHINI KUUSIKIA
New Music Nay wa mitego - Shika Adabu Yako | Download Mp3
No comments:
Post a Comment