Rais Dkt John Pombe Joseph
Magufuli akimpa pole Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Freredick Sumaye
alipokwenda kumjulia hali katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete
katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam leo Jumatatu
Januari 11, 2016.
Rais Dkt John Pombe Joseph
Magufuli akiongea na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Freredick Sumaye na Mama
Esther Sumaye alipokwenda kumjulia hali katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya
Kikwete katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam leo
Jumatatu Januari 11, 2016.
Rais Magufuli akimuaga Sumaye.
Tangu juzi kumekuwa
na ripoti mfululizo kwenye vyombo vya habari kuhusu kuumwa na kulazwa
kwa Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye katika hospitali ya Muhimbili
Leo Rais Magufuli amefunga safari
kuelekea katika hospitali ya Muhimbili kwenda kumjulia hali mzee Sumaye
japokuwa hata yeye mwenyewe hakuwa na taarifa ya ujio wa ugeni wa Rais.
“Nimeshukuru sana
Rais kuja kunitembelea hapa ni jambo kubwa, nimeshtuka kwa sababu
sikutegemeana sikupata taarifa yoyote…. namshukuru Rais Magufuli kwa
upendo wake, anaonesha kujali sana watu wake.” Amesema Frederick Sumaye na kuongeza;
“Naendelea vizuri, hali yangu ni nzuri natumaini baada ya muda mfupi nitatoka hospitali”
(Picha na Ikulu)
No comments:
Post a Comment