Nahodha
Mpya wa Taifa Stars na mshambuliaji wa TP Mazembe ya Congo, Mbwana Ally
Samatta akimuonesha Rais Mstaafu wa Awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Jakaya Kikwete tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa
wachezaji wa ndani aliyoipata usiku wa kuamkia juzi Abuja, Nigeria.
Hafla imefanyika leo kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Lumumba jijini Dar. Kikwete
(katikati) akitoa neno la kumpongeza Mbwana Samatta kwa kunyakua tuzo
hiyo, Kulia ni Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Moses Nnauye
na kushoto ni Mbwana Samatta.Baadhi ya waandishi wa habari waliokuwepo kwenye hafla hiyo leo. Nyota
wa Soka wa Tanzania, aliyeshinda Tuzo ya mwanasoka Bora wa Afrika kwa
Wachezaji wa ndani, Mbwana Samatta, akimkabidhi Mwenyekiti wa CCM, Rais
Mstaafu Kikwete, aliyokuwa akiitumia katika timu ya TP Mazeembe ya Congo
DRC, katika hafla ya Kikwete iliyofanyika leo katika Ofisi Ndogo ya
Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, kwa ajili yaRais huyo
mstaafu kumpongeza kufuatia kutwaa tuzo hiyo.Mwenyekiti
wa CCM, Rais Mstaafu, Kikwete akizungumza na kumpongeza Nyota wa Soka
Tanzania, aliyeshinda Tuzo ya mwanasoka Bora wa Afrika kwa Wachezaji wa
ndani, Mbwana Samatta (kushoto), alipozungumza na waandishi wa habari
baada ya kutana na mchezaji huyo leo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu
ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, kwa ajili ya kumpongeza kufuatia kutwaa
tuzo hiyo. Kulia ni Waziri Nape.Mwenyekiti
wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete akiwa ukumbini na Nyota wa Soka
Tanzania, aliyeshinda Tuzo ya mwanasoka Bora wa Afrika kwa Wachezaji wa
ndani, Mbwana Samatta, alipokutana na mchezaji huyo leo, katika Ofisi
Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, kwa ajili ya
kumpongeza kufuatia kutwaa tuzo hiyo.Waziri
wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, ambaye pia ni Katibu wa NEC,
Itikadi na uenezi, Nape Nnauye akimkaribisha Kikwete kuzungumza na
waandishi wa habari, katika hafla hiyo ya kumpongeza Samatta. Waziri Nape Nnauye akizungumza jambo. Wanahabari wakichukua matukio.
Kikwete na Samatta wakiongozana kutoka ndani ya Ofisi za CCM, Lumumba jijini Dar. …Akiagana na Viongozi hao.…Samatta akiondoka Ofisini hapo…Akielekea kwenye gari ili aondoke.…Akipanda kwenye gari tayari kwa kuondoka Lumumba.
RAIS wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete, leo amekutana na
mwanasoka Mbwana Samatta ambaye anaendelea kupokea pongezi za Watanzania
kwa ushujaa wa kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika kwa wale wanaocheza
soka ndani ya Afrika mwishoni mwa wiki iliyopita.Kikwete na Samatta wakiongozana kutoka ndani ya Ofisi za CCM, Lumumba jijini Dar. …Akiagana na Viongozi hao.…Samatta akiondoka Ofisini hapo…Akielekea kwenye gari ili aondoke.…Akipanda kwenye gari tayari kwa kuondoka Lumumba.
Rais huyo mstaafu amempongeza kwa mafanikio hayo lakini akatoboa siri kuwa yote ni matokeo ya wosia aliompa walipokutana jijini Kinshasa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo alimtaka awaze mafanikio ya juu zaidi hasa kucheza Ulaya badala ya kujiona kama amefika akiwa na kikosi cha TP Mazembe.
Katika mkutano na waadishi wa habari uliofanyika makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, Kikwete alisema ana kila sababu ya kumpongeza mshambuliaji huyo ambaye anaelekea kwenda kucheza soka katika klabu ya Genk ya Ubelgiji kwani ndiye mkombozi wa taifa ambalo limekuwa na ukame kwenye michezo huku akiiomba wizara husika ya michezo kuhakikisha wanamsaidia katika kila hatua.
“Tanzania tumekosa furaha muda mrefu kwenye michezo, tumekosa makombe miaka mingi, lakini Samatta leo hii ametuinua kwa kuleta tuzo hii. Lazima tumpongeze.
“Nilikutana naye Kinshasa ambako nilimisihi sana alenge juu zaidi na sio Mazembe tu na shabaha kubwa iwe ni Ulaya ili nasi siku moja tumuone kwenye runinga akicheka na nyavu. Alitekeleza nilichomwambia na kweli timu nyingi leo hii zinamtaka huko Ulaya. Nimeomba wizara ya michezo waone jinsi ya kumsaidia katika kila hatua atakayopiga,” alisema kiongozi huyo wa zamani.
Kwa upande wa Samatta amempongeza Kikwete na serikali yake ya awamu ya nne kwa kuwa naye bega kwa bega kwa kila hatua aliyoipiga.
Aidha Samatta alimkabidhi JK zawadi ya jezi ya TP Mazembe Na. 9 aliyokuwa akivaa klabuni hapo ambayo anaiacha baada ya kupata dili Ubelgiji anakoelekea sasa.
PICHA NA MUSA MATEJA/GP
No comments:
Post a Comment