Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole
Mama Maria Nyerere kufatia kufiwa na Mkwe wake Bi Leticia Nyerere
aliyefariki huko nchini Marekani. Rais alikwenda nyumbani kwa Baba wa
Taifa Msasani Dar es salaam leo Januari 11,2016 Rais Magufuli akiwapa pole wanafamilia alipofika nyumbani kwa Baba wa Taifa Msasani Dar es salaam leo.
Rais Magufuli akipata maelezo juu ya uataratibu wa msiba kutoka kwa mwanafamilia Joseph Butiku.
Rais Magufuli akipata maelezo juu ya uataratibu wa msiba kutoka kwa mwanafamilia Joseph Butiku.
Rais Magufuli akiagana na Mama
Maria Nyerere, Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,
na wanafamilia alipokwenda nyumbani kwake Msasani kumfariji kufuatia
kifo cha Mkwe wake Marehemu Leticia Nyerere huko Maryland, Marekani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 11 Januari, 2016
amemtembelea na kumpa pole mke wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere
kufuatia kifo cha Mkwewe Leticia Nyerere kilichotokea jana huko Maryland
Marekani alikopelekwa kwa ajili ya kupata matibabu mapema mwezi huu.
Pamoja na kutoa mkono wa pole kwa Mama
Maria Nyerere nyumbani kwake Msasani Jijini Dar es Salaam, Rais
Magufuli pia amewapa pole wanafamilia wote na amewaomba kuwa wavumilivu
katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na ndugu yao.
Msemaji wa familia ya Mwalimu Nyerere Bwana Joseph Butiku amemueleza
Rais Magufuli kuwa familia inaendelea na taratibu za kuusafirisha mwili
wa marehemu kutoka nchini Marekani na itatoa taarifa baadaye.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
11 Januari, 2016
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
11 Januari, 2016
No comments:
Post a Comment