Nay wa Mitego amedai amegundua mwanadada maarufu kwenye mitandao ya
kijamii, Chagga Barbie aliyekuwa mpenzi wa rapper wa Kenya, Prezzo, ni
mwanamke mwenye kila kigezo cha kuwa mama wa watoto wake.
Nay aliyekuwa akitoka kimapenzi na msanii wa filamu Shamsa Ford na
baadaye kuachana, ameiambia Bongo5 kuwa mwaka huu atafanya surprise
yoyote na mpenzi wake huyo.
“Kusema kweli mimi na Chagga Barbie tunaendana sana,” amesema. “Mimi
nina imani hata watoto wangu anaweza kuwalea. Suala la ndoa ni mpango wa
Mungu lakini naweza kusema ndani ya mwaka huu kinaweza kutokea chochote
kikubwa kwa sababu mimi natumia 966 kama codes zangu na huu mwaka ni
2016 vyote vinashabihiana. Kwahiyo naweza kusema huu mwaka utakuwa mzuri
sana kwangu,” amesisitiza.
Chagga Barbie alijipatia umaarufu baada ya skendo ya kuachana na Prezzo kwa kuchafuana kwenye mitandao ya kijamii.
No comments:
Post a Comment