Tukio la kifo cha marehemu Steven Kanumba linaendelea kumwandama
aliyekuwa mpenzi wake, Elizabeth “Lulu” Michael, kutokana na baadhi ya
Watanzania kuendeleza tabia isiyokubalika, ya kumkejeli mwanaume yeyote
anayesemekana kuwa na uhusiano naye kuwa kifo kinamuita.
Kitendo hicho kimejitokeza pia kwa muimbaji wa Nigeria, Tekno
aliyedaiwa kuwa na uhusiano naye. Hata hivyo Lulu alikanusha na kudai
kuwa huo ni uzushi kwasababu hakuna kinachoendelea kati yao.
Toka hit maker huyo wa ‘Duro’ arudi Nigeria amekuwa akipata comments
nyingi kutokana na uzushi kuwa amenasa kwenye ulimbo wa Lulu, lakini
kilichokuja kumchukiza zaidi ni comments za R.I.P zilizompelekea kuamua
kufuta picha zake zote na kuandika ujumbe mrefu kuelezea Wanigeria na
wengine wasioelewa sababu za comments za R.I.P kwenye ukurasa wake.
Haya ndio maelezo aliyopost Tekno ambayo baadae aliyafuta:
“Kwanza kabisa, ninamsamehe kila mmoja wenu aliyecomment R.I.P kwenye ukurasa wangu.
Kwa familia yangu, marafiki, bloggers na wote mliokuwa mkinipigia
kuniuliza hizo comments za R.I.P zinamaanisha nini, kuna wanaosema kuwa
nimetenda kosa la jinai nilipokuwa Tanzania! Lol.
Nilichokifanya mimi ni kupiga picha na msichana mrembo wa Tanzania
sitamtaja jina lake. Kilichotokea ni kwamba wanaume wachache ambao
waliwahi kuwa na uhusiano naye walifariki, kama wanavyosema!
Kwahiyo hawa watu wanaocomment R.I.P wanaamini kuwa nina uhusiano
naye kwasabbu ya picha niliyopost Instagram ya mimi na yeye(Lulu), hivyo
wanamaanisha na mimi nitakufa, wow! Inafurahisha.
Kwanza, nyie ni nani kuhukumu maisha yake,
Pili, nyie ni nani kucomment R.I.P kwenye ukurasa wangu…
Mungu tusamehe na utuangalie wote. Sasa mmefahamu.”
Mpaka sasa ukurasa wa Tekno una picha tano tu alizoanza kupost January 7, 2016.
Chanzo: Bongo5
No comments:
Post a Comment